0




John Walter.

Wasanii ambao kwa sasa sio wa kuwachukulia poa kwenye kiwanda cha Muziki wa Bongofleva wanazidi kuongezeka, na hii ni ishara kwamba muziki huu unazidi kukua zaidi hapa nchini lakini hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Utakubaliana nami kwamba kila kukicha kunazaliwa vipaji vipya vya waimbaji wa huu muziki lakini jitihada binafsi ndo zitafanya Vipaji hivyo viweze kufika kwa hadhara kwa urahisi.

Muziki mzuri unaongea kwa namna ya mapokezi kwa mashabiki na uzuri ni kuwa kama kazi ni mbovu watu hawakufichi wanakuchana.

Wapo wasanii kadhaa hapa nchini ambao wanapaswa kuangaliwa kwa uzito wao,kwa uandishi wao na kwa usasa wao.

Orodha ya wasanii hao ni pamoja na Wanee ambaye kwa sasa ametoa kazi mpya inayokwenda kwa jina "UTAWEZA"WANEE

Mwamba Mwingine ambaye pia ni mtayarishaji wa Muziki (pruducer) Noti Aigo anazidi kuonesha uwezo wake ambapo kwa sasa anatamba na Amapiano inayoitwa "UTANI" bonge moja la ngoma UTANI

Kijana mwingine anaesafiri kila siku kutafuta upenyo ni Daillan ambaye amefanya kazi na Mr. Blue inaitwa "HAWAPENDI" HAWAPENDI

Msanii mwingine mwenye kipaji cha kuzaliwa anaitwa Moha na kazi inajulikana kama "NIMEDATA" MOHA

Yupo jamaa mwingine anakwenda kwa jina la Mono Africano ni almasi mchangani ,kazi yake inaitwa "KAUA" KAUA

Msanii mwingine ambaye ana uhakika na anachokifanya ni Amo Dreamer ambaye ndoto zake ni kubwa kwenye Muziki, kazi yake ya hivi karibuni hii hapa inaitwa "UTANIUMIZA" UTANIUMIZA

Hajawahi kufeli mbali na mishe mishe kibao ,hapa namzungumzia Kucha Mbovu amabye amaekuwa akiendesha harakati zake yeye,Moha na CMP Kwa sasa ana mzigo mpya ameshirikiana na wasanii kibao ndani yake inakwenda kwa jina la "HATUNA UBAYA NAO" KUCHA MBOVU

Mwingine ambaye ana hasira na Kb Manyara ambaye yupo mjini na ngoma inayoitwa "MUDA"KB MANYARA

Ommy Dazzen ni mwamba mwingine anayepambana kupata upenyo kwenye muziki huu, kazi yake hii hapa "WASHA" WASHA

Silver nyota kama lilivyo jina lake ana nyota kubwa sana katika mziki huu,anahitaji kuungwa mkono tu kuweza kutoka SILVER NYOTA

Stanza kika ni mwanadada anayesafiri kutafuta upenyo STANZA KIKA

Lakini pia hatuwezi kuacha kumtaja Young Choice anaepambana kwenye jua ana mvua YOUNG CHOICE

Kwa wasanii wengine zaidi unaowaamini weka maoni yako hapa chini.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top