0

 

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Bamako ya Mali katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Yanga imezidisha matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na alama ilizokusanya hadi sasa.

Yanga ambayo imecheza mechi nne za makundi imekusanya alama saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja na kufungwa moja, huku ikiwa inaendelea kushika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi D.

 

Mabao mawili ya mchezo wa leo dhidi ya Bamako yalifungwa Fiston Mayele aliyeingia kambani katika dakika ya nane kabla ya Jesus Moloko kuzamisha jahazi la Real Bamako katika dakika ya 68.

 

Mbali ya kufunga bao, Mayele pia alifanyiwa madhambi yaliyozaa penalti ambayo ilipigwa na Yannick Bangala na kupaisha juu.

 

Wapinzani wa karibu wa Yanga kwa sasa ni TP Mazembe ambayo ina alama tatu ikishika nafasi ya tatu, huku timu zote zikiwa zimebakisha mechi mbili za kuamua kufuzu hatua ya robo fainali.

 

Ikiwa Mazembe itashinda dhidi ya Real Bamako ugenini na pia kuifunga Yanga ambayo itakuwa imefikisha alama tisa ambazo Yanga itazifikia baada ya kushinda mechi moja ijayo.

 

Hivyo ili kuwa salama Yanga itatakiwa kushinda mechi mbili zijazo kuanzia ile ya US Monastir inayotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Mkapa, Machi 19, kisha dhidi ya TP Mazembe ugenini Aprili 2.

 

Hadi sasa kwenye kundi D ambapo Yanga ipo US Monastir ndio inaongoza ikiwa na alama 10, Yanga ikiwa nafasi ya pili kwa alama saba, TP Mazembe ni ya tatu ikiwa na alama tatu ilhali Real Bamako  inashika mkia ikiwa na alama mbili, lakini bado timu zote zina nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ikiwa zitachanga vyema karata kwenye mechi mbili za mwisho.

 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top