0


Kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara utakaozikutanisha timu za singida Black stars na Fountain gate fc Oktoba 25,2024, mashabiki wa timu ya Fountain gate fc Royal fans Babati wameahidi kuibuka na ushindi kwani wamejiandaa vyema kuishabikia timu yao kwa nguvu  na kuhakikisha inapata ushindi.

Wakizindua kampeni hiyo katika mtaa wa Nakwa waliyoipa jina la "PACHA KAUTAKA" wakiwa wamepanda Punda huku mashabiki wengine wakiwa juu ya mkokoteni unaovutwa na punda, viongozi wa mashabiki hao wenye mbwembwe kibao wamesema lazima  kama pacha achapwe kwenye uwanja wao wa Nyumbani (CCM LITI).

Mwenyekiti wa tawi hilo Emmanuel Hondi amesema wanatumia usafiri wa punda kama ilivyo utamaduni wa watu wa singida ikiwa ni ishara ya kuijiandaa vilivyo kukabiliana na singida Black stars.

Kwa upande wa msemaji wa tawi hilo Nickson Sawe amesema watawauliza singida maswali matatu kuwa punda ni chombo Cha usafiri au ni mnyama kazi au ni kitoweo? na majibu yote watayapata ndani ya dakika 90.

Aidha msemaji ameongeza kuwa msafara wa kuelekea singida utajumuisha magari zaidi ya 15 na kwenda kuwaonesha singida umuhimu wa mashabiki uwanjani na namna ya kushangilia.

Fountain gate fc ni timu inayoshiriki ligi kuu ya NBC Tanzania bara yenye makazi yake mkoa wa Manyara na kwasasa inashikilia nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama 16 ikipoteza michezo miwili na kusare mchezo mmoja.

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa CCM Liti Mjini Singida saa nane kamili mchana.

Chai ya moto kikombe cha Bati ni kaulimbiu ya tawi hilo mama la Fountain Gate Fc lililopo mtaa wa Oster bay Mjini Babati.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top