WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, amewapongeza Watanzania nchini kote kwa mwitikio wao mkubwa wa kulipa
kodi mbalimbali ikiwemo ya majengo kwa hiari, hatua ambayo itaiongezea Serikali
uwezo wa kuwahudumia kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo
alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwal. J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini
Dar es Salaam.
Ametoa wito kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania
TRA kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa
maendeleo ya Taifa pamoja na kuwahimiza wananchi kudai risiti wanapofanya
manunuzi halkadhalika wafanyabiashara kutoa risiti wanapouza bidhaa kwa mujibu
wa sheria za nchi.
Baadhi ya wananchi waliofurika kulipa
kodi mbalimbali hususan za majengo katika viwanja hivyo vya Sabasaba, wameeleza
kuwa mwitikio na hamasa kubwa waliyonayo ya kulipa kodi inatokana na imani yao
kwa Serikali ya Awamu ya Tano jinsi inavyosimamia maendeleo ya nchi kwa umakini
mkubwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni