0



Watu wawili mjini Babati  mkoani  Manyara wamepoteza maisha  kwa matukio mawili tofauti  ikiwemo  mtoto wa miaka nane mwanafunzi wa darasa la pili kujinyonga kwa kamba ya manila.

 Tukio la kwanza Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Mohamedi Amiri shabani amefia katika kituo cha polisi baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya kichwani na kuvuja damu nyingi na kijana aliekuwepo katika  mahabusu Bura Malireh miaka 19 mkulima na mkazi wa kijiji cha  Gijedabou wilayani Babati mkoani Manyara aliejulikana kwa jina Bura Malireh.

Taarifa zinaeleza kuwa kijana huyo alikuwa akimdai shilingi laki mbili za za kazi ya ujenzi wa nyumba ya askari polisi  mtaa wa Kwere  aliejulikana kwa jina la Justin wa kituo cha Babati mjini  amelewa  la elekwa na mama yake kwa usalama wake.

Akizungumza na kituo hiki mama wa kijana huyo aliepoteza maisha alisema kuwa anashangazwa sana na tukio hilo huku akisisitiza kuwa  hawezi kuuchukua mwili huo atauacha hata mwezi mzima anawaachia jeshi la polisi.

“Niliondoka saa nane baada ya kuleta chakula askari akanisitizia kuwa ikifika saa 12 nisikose,ndipo niliporudi muda huo  kama alivyonielekeza,cha ajabu nafika naona wote wananishangaa nikapatwa na mstuko kisha askari akanieleza  kwamba mwanangu amepigana na mahabusu mwenzake ameumia amepelekwa hospitali ya  Mrara,kufika hospitalini hapo  getini askari ananieleza  kijana wako yupo Mochwari”alisema mama huyo huku akitokwa na machozi.

Naye baba mzazi mzee Amiri Shabani anasema kuwa amesikitishwa na tukio hilo la mtoto wake kupigwa na kuuawa akiamini kuwa limetekelezwa na askari huyo aliekuwa anadaiwa na marehem.

“Jeshi la polisi walilofanya sio sahihi ni uzembe mkubwa au ni wao wanahusika na kifo chake,haiwezekani mtu aletwe sehem ya ya usalama kisha apigwe na wao wapo. Alisema huku akiwa na huzuni.

Kwa upande wa mashuhuda walioshuhudia tukio katika kituo hicho cha polisi Babati wanasema kuwa “tulikuwa tumekaa kwenye Fomu tukisubiri kuhudumiwa, tulilichosikia ni kishindo mara mbili mfululizo na kelele za askari aliekuwepo ndani ndipo askari huyo kufika ndani ya mahabusu hiyo na kukuta huyo kijana alieletwa na mama yake akiwa amelewa  tayari ameshajeruhiwa na mahabusu mwenzake  sehem za kichwani mwake damu zikiwa zinatiririka ndipo akachukuliwa na kupelekwa hospitali” kipigo chake kilikuwa ni saa kumi jioni, Waliosema mashuhuda.  

Waliongeza kuwa baada ya mtu huyo kufanya tukio hilo alitamba na kueleza huyo tayari mleteni mwingine, hata mumpeleke hospitali gani hawezi kupona ,akawaambia askari nipigeni chuma,niue”.waliongeza mashuda waliokuwepo hapo kituoni.

Nao majirani wa marehem wakizungumza na gazeti hili  walidai kuwa alianza kupigwa tangu asubuhi na huyo askari anaedaiwa  na marehem kisha  kumpeleka  kituo cha polisi majira ya saa tano asubuhi  kwa piki piki  kama mtuhumiwa,na baadae kumwachia na kurudi nyumbani.”Tunataka kujua Kwanini alimbeba kumleta huku si mhalifu au si ana makosa kwanini  akamtoa, angemwacha aje atolewe  kituoni kwa dhamana si mhalifu, Usalama ni wapi, polisi ni  ya nini?walihoji majirani walishuhudia tukio hilo.

Waliendelea kueleza kuwa ‘baada ya kurudi nyumbani Mohamedi Amiri ambae kwa sasa ni marehem aliamua kunywa pombe huku akisikika akisema kwanini ninyimwe haki yangu bora niuawe au nijiue mwenyewe hali iliyompa wasi wasi mama yake na kuamua kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi alipoamini kuwa itakuwa ni sehem ya usalama kwa kijana wake.

Kamanda wa polisi mkoa wa  Manyara Francis Masawe akielezea tukio hilo alikiri kupokelewa kwa  kijana huyo kituoni hapo na mama yake mzazi baada ya kuleta fujo nyumbani ambapo walimfungulia mashtaka ya kutishia kujiua.

Kamanda Masawe alisema kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo ni Bura Malireh [19] na anashtakiwa kwa kosa la mauaji na kumjeruhi askari alieingia kusuluhisha ugomvi huo.

Alisema baada ya tukio hilo walimchukua Mohamedi na kumkimbiza katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Babati Mrara na akafariki wakati akiendelea kutibiwa.

“Alivyowekwa Lokapu akakorofishana huko na mahabusu wengine huko ndani na sisi tulivyopata taarifa tukamtoa na kumpeleka hospitali na bahati mbaya akafariki”.alisema kamanda Masawe.

Kijana Mohamedi Amiri Shabani aliepoteza maisha baada ya kupigwa na Burah Malireh katika Mahabusu ya kituo cha polisi Mjini Babati.
.
Kamanda wa polisi mkoani Manyara Francis Masawe amesema kuwa kijana huyo alikorofishana na wenzake huko mahabusu alipokuwa amewekwa kwa ajili ya usalama wake baada ya kutishia kujiua nyumbani kwao na mama yake kuamua kumpeleka kituoni..
Familia ya marehem inaeleza kuwa haijaridhishwa na majibu ya jeshi la polisi kuwa mahabusu ndiye aliemuua ndugu yao.
Wameeleza kuwa hawatauchukua mwili huo hospitalini hapo.
Majibu ya uchunguzi wa daktari [Post Moterm] yamepelekwa kwa O.C.D Babati.
Mganga mkuu Hospitali ya Mji wa Babati Mrara, Charles Mtabo anasema majibu yanaonyesha kuwa Mohamed alivunjika Mbavu tano,Bandama,Ini kupasuka na damu nyingi kuvuja ndani ya mwili.

Katika tukio lingine Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka nane mkazi wa Bagara ziwani Angel Yona aliekuwa akisoma darasa la pili katika shule ya msingi Debora English Medium Babati, alikutwa akiwa amejinyonga katika dirisha la chumbani-nyumbani kwao kwa kamba ya Manila. Tukio hilo la kusikitisha limeacha watu wengi na maswali kichwani huku wakihoji inawezekanaje mtoto mdogo kiasi hicho aweze kujiua.


Jeshi la polisi mkoani Manyara bado linaendelea na uchunguzi juu ya matukio hayo mawili ya kusikitisha.




Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top