Mwanamuziki
wa Bongo fleva Ali Kiba anayeendelea kufanya vyema na ngoma yake ya
‘Mvumo wa Radi, atapimana nguvu na mchezo soka la kulipwa Mbwana Samatta
uwanja wa Taifa.
Ali Kiba amajulikana kwa uwezo wa kucheza mpira
uwanjani na alikwisha weka wazi kuwa ana mapenzi mazito kwa mpira wa
miguu na hata kusema asingekuwa msanii basi siku nyingii angekuwa mcheza
mpira.
Kwa
mara ya kwanza uwezo wa kusakata soka ulionekana Kwenye mechi
iliyohusisha wasanii wa Bongo fleva na wasanii wa Bongo movie miaka ya
nyuma kidogo.
Habari njema kwa mashabiki zake ni kuwa utamshuhudia
Ali Kiba Live kunako dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
tarehe 9 juni mwaka huu akiwa na Mshambuliaji wa timu ya taifa na klabu
ya KRC Genk, Mbwana Samatta.
Ali Kiba ametangaza Habari hiyo njema kwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika ujumbe huu:
Tukutane Taifa naomba unichagulie kikosi bora unacho kikubali kutoka team tofauti katika ligi ya TANZANIA bara.
Wawili
hao watakutana kwenye mechi maalumu ya ubalozi wa kujitolea ili
kuchangia elimu, hata hivyo orodha ya majina mengine ya wasanii
yataendelea kutajwa kadri ya siku zinavyokwenda.
Mbwana Samatta ameandika ujumbe huu kutjibitisha kuwepo katika pambano hilo:
Nimepewa jukumu la kuandaa jeshi la maangamizi mchezaji gani ungependa kumuona siku iyo awe wa sasa au wa zamani?
Post a Comment
karibu kwa maoni