Shule ya
msingi komoto iliyopo mtaa wa Komoto halmashauri ya mji wa Babati mkoani
Manyara inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa matundu ya
vyoo,ofisi ya walimu na nyumba za walimu.
Akizungumza
na redio manyara mapema leo ofisini
kwake mkuu wa shule hiyo mwalimu Eroyano ameeleza kuwa licha ya changamoto hizo
pia wanafunzi hawapati chakula cha mchana shuleni hapo kutokana na wazazi kuwa na muamko mdogo
katika kuchangia hali inayoilazimu shule kuwaruhusu wanafunzi wakale majumbani
wakati wa mchana na kurudi shuleni.
Mkuu huyo
ameitaka serikali ya mtaa wa Komoto na Halmashauri ya mji kwa ujumla kuweza
kutatua changamoto hizo mapema ili wanafunzi waweze kupata elimu katika ubora
na kuwapa walimu hari katika kufundisha.
Katika hatua
nyingine Eriyano ameelezza kuwa katika shule yake wanafunzi 47 waliosajiliwa
kwenye baraza la mitihani kufanya mtihani wa darasa la saba ni mwanafunzi mmoja
mvulana ambaye alitoroka nyumbani kwao
tangu mwezi march mwaka huu na kwenda kusikojulikana.
Mkuu huyo
ameeleza kuwa pia wanakabiliwa na uhaba wa ofisi za walimu hali inayowalazimu
kutumia moja kati ya madarasa kama ofisi huku kukiwa miundo mbinu chakavu ya
vyoo kwa upande wa wavulana.
Naye mwalimu
Nuru amekiri kuwepo kwa changamoto hizo shuleni hapo na kuitaka serikali iweze
kuwatatulia kwa haraka zaidi.
Mapema mwaka
huu Fedha za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya shule za
msingi na sekondari ikiwemo malipo ya ada mkoani Manyara,ambapo ilionekana
kuzua utata wa matumizi yake hususani katika shule za msingi kutokana na
mahitaji mengine kukwama hasa yale yaliyokuwa yakitegemea mchango wa jamii.
Utafiti wa hivi karibuni
ulibaini changamoto za matumizi ya fedha
hizo kuwa ziko katika shule za msingi
huku sekondari za kutwa zikikabiliwa na changamoto ya wazazi kugomea mchango wa
chakula.
Mkoa wa
Manyara wenye shule za msingi 619 zenye wanafunzi 246.000, zimepatiwa ruzuku ya
zaidi ya shilingi 295,778,000/=
Na zaidi
shilingi 293,748,000/= zikipelekwa kwa shule za sekondari 135 zenye idadi ya
wanafunzi 46,600.
Katika moja
ya shule ya Msingi Komoto, iliyoko mjini Babati ambayo imepokea mgao wa zaidi
ya shilingi laki mbili kwa kipindi cha January hii, imeonekana fedha hizo
kutokidhi mahitaji mengine.
Post a Comment
karibu kwa maoni