BABATI
MANYARA
Serikali
imeombwa kushusha gharama za nishati ili bidhaa mbalimbali hapa nchini viwanda
vinavyozalisha bidhaa mbali mbali ziweze kuuzaa bidhaa zao kwa kwa bei wananchi watakazoweza kuzimudu.
Hayo
yameelezwa na meneja wa mauzo wa kampuni ya saruji ya tanga sementi taifa
bw;leslie masawe katika semina ya siku1 kwa wadau wa ujenzi mjin babati mkoani
manyara.
Hata hivyo
bw masawe amesema kwa sasa kiwanda hicho kinatumia nishati ya joto ya makaa ya
mawe ambayo inapatikana mkoani iringa umbali wa km zaidi ya 200 suala ambalo
bado ni changa moto kubwa kwa kiwanda hicho.
Aidha
ameoeongeza kuwa endapo serikali ingefikisha nishati ya gesi mkoani Tanga
ingekuwa vyema na uafadhali kwani wangetumia nishati hiyo katika uzalishaji
kiwandani hapo na kupunguza gharama za uendeshaji.
Kauli hiyo
inakuja huku serikali kupitia TPDC ikiwa tayari imeshaweka mkakati wa kusambaza
mabomba ya gesi asilia ambayo pia kwa kaskazini litapita mkoani Tanga.
Akitoa
semina ya siku moja mhandisi wa Petroli Tanzania [TPDC] Felix Nanguka ameeleza
kuwa mradi huo wa gesi asilia serikali itakuwa na asilimia 20 akiwa kama
mshirika.
Kwa Tanzania
ugunduzi wa Gesi asilia mpaka sasa ni
Trioni 57.25% nyingi ikiwa ni kutika katika ukanda wa Maziwa na Bahari.
Hata
hivyo kampuni ya Tanga sementi
imeanzisha bidhaa mbalimbali mpya za
simenti huku hivi sasa ikiingiza simenti yenye ujazo kama ule wa Simba siment
yenye jina Mkombozi simenti ya mwendo
kasi yenye ubora na gharama nafuu inayoendana na maisha ya
Mtanzania pamoja na nyingine ambayo ni mahususi kwa ajili ya ujenzi wa bara
bara.
Katika
mafunzo hayo Masawe aliwafundisha wadau hao wa Saruji mkoa wa Manyara mbinu
za ujenzi kwa kutumia sementi vizuri ili kuepuka kupasuka na kubomoka
kwa nyumba nakuongeza kuwa uzingatiaji viwango vya ujenzi ili kuepusha kubomoka
kwa nyumba hata kipindi cha maafa kama ya tetyemeko la ardhi kama
yaliyovyotokea huko mkoani Kagera na kusababisha nyumba nyingi kubomoka.
Post a Comment
karibu kwa maoni