0

Wananchi wa Kijiji cha Nyabiyoko Katika Kata ya Bwanja Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera wamekumbwa na Taharuki kufuatia  Moto ulioonekana kutoka Chini ya  ardhi hali iliyowasababishia  hofu ya kutokea kwa Mlipuko wa Volkano.
Wakizungumza na Mwandishi wa kituo hiki kutoka eneo LA tukio baadhi ya Wananchi hao ni Pamoja na Valelia Mombeki na Visenti  Timanywa wamesema kuwa tukio LA moto huo kutoka chini ya ardhi umetokea jaribu na Shule ya Msingi  Katarabuga katika Wilaya hyo ya Missenyi.
Wamesema kuwa Moto huo ulianza katika eneo Dogo na kadili siku iliyofuata moto huo ulizidi kutapakaa hali ambayo walijawa na hofu wakidhani kuwa ni Mripuko huo wa Volkano.
Kwa u pande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania Profesa Abdukalimu Mruma  amewatoa hofu Wananchi wa Eneo hilo na kusema Volkano haiwezi kutoka katika eneo hilo kwamba huenda kuna MTU alirusha moto kwenye eneo hilo na kusababisha hali hiyo kwani hali hyo hutokea kutokana na kuwepo kwa Udongo uliojaa Masalia ya miti namimea Mbalimbali na kusisitiza kuwa Volkano huwa inatokea kwenye hali ya Majimaji na hali ya kuwa na Joto jingi.
Nae Mkuu wa Wilaya hiyo ya Missenyi Mkoani Kagera Ruteni Kanali Denis Mwila amewataka Wananchi wa Wilaya hyo ya Missenyi kutokuwa na Taharuki na Badala take Wfuate Ushauri wa wataalamu wa Mianba ambao wanatoa Maelekezo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top