Ikiwa
ni mwezi mmoja tangu rais Magufuli wakati akizungumza na wahariri wa
vyombo vya habari kusema kuwa kwa sasa anachofanya ni kuinyoosha nchi na
kujenga uchumi hivyo mchakato wa katiba usubiri, kauli hiyo iliibua
hoja mbalimbali huku wengine wakisema mchakato huo wa katiba sasa
umekwama, waziri Mwakyembe anafafanua.
Kauli
hiyo inakuja ikiwa ripoti ya utafiti juu ya uelewa wa wananchi kuhusu
katiba iliyotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya OSIEA ikishirikiana
na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania iliyozinduliwa
jijini Dar es Salaam ikionesha kuwa asilimia 50 ya watanzania hawaijui
katiba ya sasa ya mwaka 1977, asilimia 74 hawajui inapatikana wapi
wakati asilimia 14 hawajui kama kuna katiba.