HOFU
imetanda wilayani Karatu katika Mkoa wa Arusha baada ya tukio la kwanza
la uchunaji ngozi kuripotiwa katika mji mdogo wa Karatu.
Binti
mdogo mwenye umri wa miaka tisa, ameuawa mjini Karatu baada ya kutekwa
nyara na watu wasiojulikana wakati akielekea machungani na mifugo.
Mtoto
huyo, Witness Andrew ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Kwanza
kwenye Shule ya Msingi ya Sumawe, alipatikana Jumatano usiku, akiwa
tayari amekufa, baada ya kuripotiwa kupotea kwa zaidi ya saa 24 tangu
alipoondoka nyumbani kwao akiwa anaswaga ng’ombe na mbuzi, Jumanne
iliyopita.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Kiwandani ambako mwili wa mtoto huyo ulipatikana,
Alexander Lulu amesema maiti ta mtoto huyo ilikutwa ikiwa imetupwa
shambani na baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa pamoja na ngozi
iliyochunwa na kuondelewa kabisa.
Witness
pia alikutwa bila mguu, mkono na sehemu zake za siri na baadhi ya
wakazi wa Kijiji cha Tloma wanadai ni masuala ya ushirikina.
Mtoto huyo
ndiye wa kwanza kuchunwa ngozi katika eneo la Karatu na tayari hofu
imeanza kutanda hapa, watu wakihofia kuwa wachuna ngozi watakuwa
wamevamia wilaya hiyo.
Baba
ya marehemu, Andrea Paulo na Mama Paulina Petro wanasema mtoto wao
alipotea tangu Jumatatu wiki hii alipotoka na mifugo kwenda kuchunga
kwenye uwanda wa Tloma, lakini hakurudi nyumbani, na kwamba mifugo
aliyokuwa nayo ilirejea yenyewe.
“Tulimtafuta
mtoto kila mahali, lakini bila mafanikio, hata tulipoikuta maiti yake
eneo la Kiwandani, tulishangaa maana tulishapita kwenye mashamba hayo
mapema, lakini hatukumuona,” walisema wazazi.
Wanakijiji
wa Tloma wanaamini kuwa mtoto huyo alitekwa na kupelekwa eneo jingine
ambako ndiko alichinjwa kabla ya wauaji wake kumrudisha na kumtupa
Kiwandani.
Post a Comment
karibu kwa maoni