Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia),
akijibu hoja zilizotolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji
Kasidi (kushoto) alipofika Ofisi Kuu ya Chuo hicho kabla ya kufungua mafunzo ya
siku nne ya wakaguzi kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi aliyesimama akitoa
utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa
wakaguzi wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa. Kushoto
kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, Mkaguzi
wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa
Kiufundi Bw. Amin Mcharo na kulia kwa Kaimu Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani
Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa.
Wakaguzi
wa Ndani kutoka Serikali za Mtaa na Sekretarieti za Mikoa wakiwa kwenye mafunzo
ya ukaguzi, Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika. Mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa
Chuo cha Uhasibu Arusha, mkoani Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (aliyesimama)
akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa ndani ambapo alisema mpaka
sasa wakaguzi wa ndani 308 wamepata mafunzo hayo na wakaguzi 32 wameshafanya
mafunzo hayo kwa vitendo.
Wakaguzi
wa Ndani kutoka Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa katika picha ya
pamoja. Waliokaa ni Mgeni Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango
Bi. Doroth Mwanyika kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt.
Faraji Kasidi, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo na
kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed Mtonga na Mkaguzi wa
Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa.
Mgeni Rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika
(katikati) wakibadilishana mawazo na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt.
Faraji Kasidi (Kushoto) na kulia ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Mohamed
Mtonga.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika akimsikiliza Mkaguzi
wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali – Ukaguzi mamlaka za mitaa Bw. Mwanyika Musa
ambapo alisema mafunzo hayo ni muhimu kwani yamelenga kuimarisha ukaguzi wa
miradi mikubwa ili ujenzi wake ulingane na thamani ya fedha iliyotumika.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi akumfafanulia jambo Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika.
Post a Comment
karibu kwa maoni