Na SAFINA SARWATT- MOSHI
MTOTO
mchanga wa siku tano amefariki dunia baada ya kufanyiwa kitendo cha
ukeketaji na bibi yake aliyejulikana kama Longida Naingola mkazi wa
Kijiji cha Naibera, wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad
Mutafungwa, kichanga hicho kutoka kabila la Wamasai kilifanyiwa kitendo
hicho cha kikatili Desemba 30, mwaka jana katika Kijiji cha Naibera,
wilayani Simanjiro.
“Mtoto
alizaliwa Desemba 25, 2016 na Desemba 30, 2016 saa 4:00 asubuhi, bibi
huyo alimkeketa na baada ya kitendo hicho hali ya mtoto ilikuwa mbaya
kutokana na kutokwa na damu nyingi sehemu zake za siri,” alisema
Mutafungwa.
Mutafungwa
alisema ilipofika Januari 11, 2017 mtoto huyo alifikishwa katika
Hospitali ya Rufaa ya KCMC akiwa na mama yake mzazi, Fatina Joshua (14).
Alisema
baada ya kufikishwa hospitalini hapo madaktari waliompokea walimkagua
na kukuta mtoto huyo akiwa ameharibika vibaya sehemu zake za siri na
ilipofika Januari 13, mwaka huu alifariki dunia.
Kamanda
Mutafungwa, alisema baada ya kupata taarifa hiyo waliwatafuta
watuhumiwa na kumkamata bibi pamoja na mama wa kichanga hicho.
Alisema
mwili wa kichanga hicho umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC
huku uchunguzi ukiendelea ili kuchukua hatua zaidi za kisheria.
Aidha,
Kamanda Mutafungwa alisema jeshi hilo pia linaendelea kushirikiana na
Jeshi la Polisi mkoani Manyara kutokana na tukio hilo kufanyika huko.
Post a Comment
karibu kwa maoni