Licha ya serikali kusisistiza wanafunzi wa shule
za msingi na sekondari kupata chakula cha mchana Shuleni baadhi ya shule
zimeshindwa kufanya hivyo kwa maelezo kuwa elimu ni Bure.
Shule nyingine hata kwenye vikao vinavyoitishwa
kwa ajili ya kuweka utaratibu wa wanafunzi kupata chakula,mwitikio kwa wazazi
umekuwa ni mdogo.
Akizungumza na kituo hiki ofisini kwake mkuu wa
shule ya Sekondari Sigino katika Halmashauri ya mji wa Babati Mkoani Manyara Bi
Leonardina Binamungu na msaidizi wake Paulo Niima wameeleza kuwa changamoto
kubwa inayokwamisha jitihada za chakula cha mchana shuleni hapo ni ukosefu wa
maji.
Kutokana na hali hiyo inawalazimu kuwaruhusu
wanafunzi saa nane za mchana hivyo kukosa masomo ya jioni pamoja na michezo na
kupelekea ufaulu kuwa mdogo.
''Katika miaka ya nyuma shuleni hapa wanafunzi
walikuwa wakipatiwa chakula cha mchana ila tangu serikali iseme hakuna wazazi
kuchangishwa,wazazi wamerudi nyuma".
"Mimi naona kuwa walipotoa sera hii kwamba
wanafunzi wasichangishwe wangetembelea
na kuangalia mazingira,sisi hapa
tunakabiliwa na tatizo la maji'. aliendelea kusema mwalimu huyo.
Binamungu amesema kuwa ruzuku inayotolewa na
serikali kwa ajili ya kutekeleza sera ya elimu Bure katika shule yake imekuwa
ni kidogo kutokana na uchache wa wanafunzi.
"Shule hii ni ndogo inapata wanafunzi
wachache,hii pesa tunayoletewa ya elimu bure ni kubwa kulingana na idadi ya
wanafunzi,sasa shule hii ina wanafunzi kidogo na pesa inayoleta ni kidogo.Kifungu
cha utawala tunapata shilingi elfu themanini na tano 85,000,kati ya hizo 60000
elfu tunalipa mlinzi,matuimzi ya maji kwa siku katika shule hii ni pipa tatu
kwa shilingi elfu 15,000".
Mkuu huyo ameiomba serikali ya Halmashauri ya mji
wa Babati na wizara husika kutatua changamoto zilizopo haswa hilo la maji ili
shule hiyo iweze kuendelea mbele.
Shule hiyo ina nyumba mbili za walimu huku walimu
wakiwa 19 ambapo katia ya hao wanaoishi
kwenye nyumba za walimu ni watano pekee kutokana na ukosefu huo wa maji.
"Mimi nafikiri ufumbuzi wa changamoto hizi
ni serikali kuleta maji ya uhakika katika shule hii".Alisema Binamungu
Katika halmashauri ya mji wa Babati shule ya
Sekondari Sigino pekee ndio inayokabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa
Maji na umeme.
Aidha ameongeza kwa kusema kwamba mpaka kufikia
tarehe 18 Januari 2017 shule ilikuwa na wanafunzi 145,kidato cha kwanza
[56]wavulana [23]wasichana [33],kidato cha pili [42] wavulana [19] wasichana
[23],Kidato cha tatu [24] wavulana [9],wasichana [18],kidato cha nne [22]
wavulana [10], wasichana [12].
Nao wanafunzi wakizungumzia adha wanayokutana
nayo kutokana na ukosefu wa huduma ya chakula cha mchana na maji,wamesema
inawafanya kufanya vibaya katika masomo yao kutokana na kukosa kwa masomo ya
jioni kwani inawalazimu kutoka shuleni mapema ili kuwahi majumbani kupata
chakula.
Kwa upande wa watoto wa kike wanasema wapo katika
hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza kutokana na kukosekana kwa maji katika
vyoo.
"Kuna muda inabidi tuache vipindi tukatafute
maji na ni umbali mrefu sana zaidi ya kilomita 5"walisema baadhi ya
wanafunzi wa kidato cha nne.
Wanafunzi hao wameiomba serikali itoe msaada
katika shule hiyo ili wapate elimu bora na kufanya michezo katika shule hiyo.
Akizungumzia hilo katika Baraza la madiwani
katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2017\2018 mkuu wa wilaya ya Babati
Raymond Mushi alisema wanaendelea kufuatilia shule ambazo hazitoi chakula cha
mchana kwa wanafunzi na kuwahamasisha wazazi kuchangia huduma hiyo.
"Chakula kwa wanafunzi ni lazima kila shule
na haihusiani na elimu bure,wazazi wanatakiwa wachangie"alisema Mushi.
Post a Comment
karibu kwa maoni