Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashari kwa ajili ya kumtambulisha kuwa kiwanja ni chake sasa hivi kiwancha hicho kinataka kunyang’anywa na halmashauri ya Wilaya ya Monduli. |
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Monduli
wameitupia lawama halmashauri ya wilaya hiyo na kusema kuwa inachochea migogoro
ya ardhi na kuwanyima baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika
vijiji vyao
Hayo wamesema jana wakati walipokuwa wakifanya
mkutano wa adhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya
kilichopo ndaniya halmashauri ya Monduli mkutano ambao
uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila
(Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka
kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa
na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao unaongozwa na chadema kwani katika
kipindi kilichopita walikuwa hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao
ambayo walikuwa wanaishi tangu enzi za mababu zao .
Mmoja wawananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la
Songoyo Ole Matata alisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa
ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo hayo ambayo ,walikaa tangu enzi za
mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi
wote bali uongozi huo unafukuza wananchi kulingana na chama ambacho anatokea.
“Tumekuja apa siku nyingi lakini tunashangazwa
hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri hii ichukuliwe na chadema tumekuwa
tunanyanyaswa sana haswa sisi tunaotoka na tunajilikana ni wanachama wa chama
cha mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu hata sisi tunaolalamika ambao tumeambiwa
tumevamia msitu ni wanachama waCCM hamna mwanachama hata mmoja wa CHADEMA
ambaye amefatwa akaambiwa amevamia msitu ,mimi mwenyewe pembeni yangu
nimepakana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo hay o
hayo kunashamba la Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu
waondoke ila sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu
kwakweli hii sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana
tunanyanyaswa sana”alisema Amina Longitoti
Akiogea katika mkutano huo Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare
alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema,
inachochea migogoro ya ardhi na chama chao hakitakaa kimya kwa
hilo.
Alisema vijana wa kimorani, Laigwanani na watu
wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji
hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki
ardhi hivyo anashangazwa na kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa
wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria.
Alisema CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa na
baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi na hatakuwa tayari kuona
wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya mtu binafsi .
“mimi nilipata shamba hilo kama mwananchi wa
kijiji hicho na sikuchukuwa shamba hilo kama kiongozi wa CCM hivyo
nashangaa sana kwa kitendo cha kuingiza chama katika mambo yangu binafsi
kimenisikitisha sana na kwakweli sita vumilia kabisa na kingine
kinachonishangaza sio mimi tu au sisi tu ndio tunamashamba au tunamiliki
ardhi katika kijiji hichi kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hili
pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema lakini
nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni sisi tu “alisema Sanare
Kwa upande mwananchi mungine aliyejitambulisha
kwa jina la Olais Taiyai alisema kuwa ubaguzi na uchochezi
uliopo ndani ya halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na hautavumilika hata
kidogo kwani sio jambo jema linalofanywa na viongozi hao na kuomba serikali
kuingilia kati swala hili kwani wananchi hao wanateseka na hawana pa
kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa katika viwanja vyao
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya
Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani huo ni
upepo mchafu unaovuma kupitia
Hivi karibuni Baraza la madiwani la Halmashauri ya
wilaya ya Monduli, lilipitisha azimio la kuchukua ardhi ya kijiji hicho kwa
madai kuwa waliochukua ardhi hiyo hawakufuata sheria, akiwemo mwenyekiti wa CCM
wa wilaya hiyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni