0


Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala, ametoa maagizo mazito kwa Vyombo vya Usalama nchini kuhakikisha vinamkamata mtu anayejulikana kwenye mitandao ya kijamii kama James Delicious kufuatia  kujitangaza kwake  kama shoga kinyume cha sheria ya Tanzania.

Dk. Kigwangalla ametoa kauli hiyo jana jioni mjini Dodoma Bungeni wakati akijibu hoja za wabunge juu ya hatua kwa mtu anayefanya vitendo hivyo ambapo ameviagiza vyombo vya usalama kumtafuta mtu huyo na iwe fundisho  kwani ni kinyume  na sheria za nchi  kwa kuendesha biashara ya kuuza ngono ya kinyume cha maumbile.

Mbali na James Delicious, wengine ambao ameagiza wajisalimishe wenyewe kituo cha Polisi Central Dar es Salaam ni pamoja na  Kaoge Mvuto na Dani Mtoto wa Mama ambao wamekuwa wakijinadai kufanya vitendo hivyo hapa nchini ambavyo ni kinyume na sheria.
 
KIGWANGALLA: Serikali kupiga Marufuku Matumizi ya Pombe za VIROBA Kufikia Mwezi wa Sita mwaka 2017.

Wakati huo huo, akiendelea kujibu maswali amebainisha kuwa Serikali itazuia viroba kutengenezwa nchini na kufuta kabisa matumizi ya pombe za aina ya viroba hapa nchini wakati akijibu hoja za wabunge kufuatia michango mbalimbali ya wabunge juu ya hoja za Kamati za UKIMWI na Madawa ya Kulevya na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya jamii.

Dk. Kigwangalla alisema, ‘haitopita mwezi wa sita Serikali itakuwa imepiga total ban (marufuku) matumizi ya madawa ya kulevya nchini….’

Miezi kadhaa iliyopita Dk. Kigwangalla aliongoza kikosi kazi cha Serikali kilichokuwa kinashughulikia suala la viroba ili kutathmini ukubwa wa tatizo na kupendekeza hatua za kuchukua.

Kikosi kazi kilibaini changamoto nyingi ikiwemo ya uwepo wa viwanda bubu na pombe zinazochanganywa na spirit ya viwandani.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top