0

Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE, CHRISTOPHER OLE SENDEKA.
 
Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE CHRISTOPHER OLE SENDEKA ametoa muda wa siku NNE kwa wakazi wa mkoa huo kupanda miti mitatu kwa kila kaya ili kuendelea kutunza mazingira ya mkoa huo.

OLE SENDEKA ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti mkoani humo katika barabara ya MAKAMBAKO - SONGEA iliyojumuisha viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa NJOMBE SHIGELA GANJA amesema zoezi la upandaji miti linakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo uwezo mdogo wa wakala wa mbegu taifa pamoja na jamii kujikita katika kuotesha miti ya kigeni.

Nao baadhi ya wakazi wa mkoa wa NJOMBE wameipongeza hatua hiyo ya mkuu wa mkoa na kusema itasaidia katika utunzaji wa mazingira mkoani humo.

Miche zaidi ya Milioni AROBAINI NA TISA imeandaliwa kwa ajili ya Kampeni hiyo ya upandaji wa miti katika mji wa NJOMBE ikiwa ni pamoja na miti ya vivuli na mapambapo ambapo viongozi wa chama cha mapinduzi CCM, wananchi, wafanyakazi wa ofisi ya mkoa pamoja na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wameshiriki katika kampeni hiyo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE OLE SENDEKA amevitaka vyama vya siasa mkoani humo kuacha kutumia nguzo za umeme za Shirika la Umeme Nchini TANESCO pamoja na miti inayopandwa kwa ajili ya kupandishia bendera zao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top