0
 
Hatimaye Miss Valentine 2017 Babati amepatikana mara baada ya kufanyika mchujo mkali uliofanyika katika ukumbi wa Manyara Country mjini Babati.
Ni mzaliwa wa Bagamoyo,ana umri wa miaka 20.
Miss Valentine Flora Robert ni mwanafunzi wa chuo cha uasibu IAA Babati tawi la Arusha alikuwa akichuana na wengine kumi na watano ambao amefanikiwa kuwabwaga chini.
Flora ameeleza sababu za yeye kushika namba moja ni maombi ambayo anayafanya mara kwa mara.
"Yaani siri ya mafanikio yangu ni maombi,huwa namshirikisha Mungu katika kila jambo nalolifanya".
Amesema kilichowaangusha wengine ni kutojiamini na kushindwa kujibu maswali kiufasaha.
Amewatia Moyo washiriki walioshindwa kwamba wasikate tamaa waendelee kumshirikisha Mungu na kujiamini kwa kila wanchokifanya.
Miss Valentine akizungumza na John Walter Blog amesema kuwa ataendelea kushiriki mashindano mengine ya Umiss yatakayojitokeza.
Kuhusu tabia za baadhi ya mamis kubadilika baada ya kushinda amesema kwamba yeye hawezi iga tabia yeyote ambayo ipo kinyume na maadili katika jamii.
Ametoa shkrani zake kwa mama yake kwa kumlea na kushauri vizuri"Namshukuru sana Mama yangu amenilea vizuri na kunishauri mengi akinitaka nijiamini."alisema Miss Flora Robert.
Sasa ataonekana siku ya Valentine katika mwonekano wa kipekee akiwa amevalia nguo nyekundu.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top