Tarehe kama ya leo mwanamuziki wa Tanzania Moses Bushagama maarufu kama Mez B alifariki dunia.
Mez B aliyekuwa mmoja wa wanamziki wanaounda kundi la Chamber squard,alifariki tarehe 20 Februari 2015 mjini Dodoma kwa ugonjwa wa homa ya mapafu(TB).
Mez B anakumbukwa kwa vibao vyake vikali kama Kikuku, kama vipi, nimekubali na nyimbo ya Ghetto langu aliyoshirikishwa na Marehemu Albert Mangwea.
Huyu ni msanii wa pili kufariki kutoka kundi la chamber squad imepoteza wasanii wake wawili.Kabla ya Mez b Kufariki Miaka miwili iliyopita kundi hilo liliomboleza kifo cha mwenzao Albert Mangwea a.k.a Ngair ambapo Mez B alikuwa mstari wa mbele wakati wa mazishi yake.
Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi Amen.
Post a Comment
karibu kwa maoni