
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama hicho, Anatropia Theonist, ambapo amesema kuwa viongozi wa Chadema watakwenda kusherekea Pasaka Gerezani.
Amesema kuwa kuendelea kuwepo Mahabusu kwa Mwenyekiti wa Chama hicho kimewafanya viongozi wengi wa Chama hicho kwenda kusherekea sikukuu ya Pasaka Gerezani.
“Tutawabebea zawadi za Pasaka ikiwemo vyakula viongozi wetu hawa, tutaanzia Gereza la Segerea baada ya kuwaona kila mmoja ataenda kwake kumalizia sherehe,”amesema Anatropia
Aidha, amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na viongozi wengi wa chama hicho kuwekwa rumande hivyo, njia bora ya kuwafariji ni kuwatembelea.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.