Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu nchini imevitaka vyombo vya kisheria na
uchunguzi kuacha kupuuza kauli zilizotolewa na wabunge zilizomtuhumu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumiliki mali zisizoendana
na kipato chake halali.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji wa
Jumuiya hiyo Sheikh Rajabu Katimba, alisema wakati wa mkutano wa Bunge
lililopita baadhi ya wabunge walimtuhumu Makonda hivyo tuhuma hizo
zinapaswa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.
Alisema
vyombo vyenye mamlaka ya uchunguzi vinapaswa kufanya uhakiki wa mali
za Makonda ili kuondoa shaka katika umiliki wa mali aliyonayo na uhalali
wa misaada ya kifedha zinazotolewa kwake na taasisi rafiki.
Sheikh
Katimba alisema kifungu cha (11) cha sheria ya maadili ya viongozi wa
umma inamtaka kiongozi kutaja hadharani mali zake ikiwemo zawadi
anazopewa.
Hivi
karibuni, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) wakati akichangia
taarifa za Kamati ya Bunge na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alisema
Makonda amenunua jengo ‘(Apartment ) lenye thamani ya shilingi mil 600
jijini Dar es Salaam.
Selesini
aliliambia Bunge kuwa Makonda amempa gari mkewe aina ya Mercedez Benzi
lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh milioni
550.
Mbali
na Selesini, Mbunge mwingine aliyemtuhumu Makonda kujilimbikizia mali
ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) ambaye naye wakati
akizungumza bungeni alihoji ni wapi Makonda alipata fedha za kusafiri
kwenye ndege daraja la juu kwenda Marekani.
Wakati huo huo, Sheikh Katimba alisema vita dhidi ya dawa za kulevya inaweza kwenda vibaya iwapo itasimamiwa na wanasiasa.
Alisema ili kuepuka hilo vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kisheria vinapaswa kuifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.
Sheikh
Katimba alisema taasisi za kiislamu zinaunga mkono jitihada
zinazofanywa na Serikali kupambana na biashara hiyo na kusisitiza kuwa
vyombo vyenye mamlaka kuisimamia kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na
Kupambana Dawa za Kulevya nchini ya mwaka 2014.
‘’Hatuoni
ni kwa mantiki ipi watumiaji wengine washitakiwe kwa kutumia dawa na
wengine waachiwe huku zitumike na fedha za kuwatibia nje ya nchi.
‘’Wasanii
kama Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la Ray C’ msanii TID nao pia
walipaswa kushitakiwa kama walivyofanywa wengine na vilevile watumiaji
walioko mitaani na kwenye vituo vya daladala wote wasombwe wakapimwe na
kisha washitakiwe.
“Pamoja
na nia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuongoza na
kuendesha vita hiyo lakini vita isimamiwe na vyombo vyenye weledi na si
wateule wa kisiasa au wanasiasa,’’ alisema.
Aidha,
alizungumza kesi za ugaidi inawakabili baadhi ya viongozi wa dini kwa
kueleza kuwa haitakuwa na tija wala heshima iwapo viongozi hao
wataendelea kushikiliwa gerezani.
“Ni
kweli serikali inatutaka tuiunge mkono kwenye vita hiyo nasi tuko
tayari lakini ni vuziri jitihada hii ikawa kwa watu wote, tunaiona
serikali inashindwa kutenda haki kwa viongozi wa dini yetu na ni kesi
gani isiyokwisha? inatia aibu masheikh kufungwa bila hatia miaka mitatu
ni sawa na kufungwa bila hatia,’’ alisema Sheikh Katimba.
Post a Comment
karibu kwa maoni