0
 
Wakati vita ya madawa ya kulevya ikiendelea hapa nchini,mkoa wa Manyara kupitia jeshi la polisi limeanza operesheni kali ya kutafuta wahalifu mbalimbali wakiwemo watumiaji wa madawa hayo na wauzaji.
Vita hiyo aliyoitangaza rais Magufuli na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuanza nayo imeungwa mkono na watu wengi hapa nchi wakiwemo viongozi wa kidini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za jeshi hilo mnadhimu [ACP] Longinus A.Tibishubwamu amesema kuwa Operseheni hiyo ni endelevu na imeanza kwa kuwakamata watu watatu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa bangi huku mmoja akikutwa na coceine na wengine zaidi ya ishirini kwa kosa la uzururaji wakati wa usiku.
Amewataja waliokamatwa na madawa hayo kuwa ni Cecilia Alex maarufu kama Mama Chichi miaka 45 mkazi wa Osterbay Babati mjini [ misokoto 24 ya bangi] Issa Mstafa ambaye ni fundi viatu mkazi wa Osterbay, miaka 27 hao ni wauzaji na  watumiaji  pamoja na Hemedi Ali, miaka 30 mkazi wa Komoto aliekutwa na kete nne za madawa ya kulevya yanayodhaniwa kuwa ni Kokeini.
Aidha Tibishubwamu ameeleza watu hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayo wakabili.
Kwaupande mwingine akizungumzia swala laulinzi na usalama katika mkoa wa manyara unazidi kuimarishwa zaidi ambapo kwa sasa wameeandaa kikosi maalumu kinacho fanya doria usiku na mchana katika wilaya zote za Mkoa wa Manyara .
Kikosi hicho maalumu katika gari wanayoitumia imewekwa Rungu mbele na nembo iliyoandikwa kwa maandishi makubwa SIMBA DUME.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top