Baada
ya sauti zilizosambaa zikimuhusisha Mwigizaji Steve Nyerere na Mama wa
mwigizaji Wema Sepetu wakizungumza huku akitaja baadhi ya viongozi
mbalimbali aliodili nao kwenye sakata la Wema kushikwa na Polisi, leo
Steve Nyerere ameita Waandishi wa habari na kuongea nao.
Steve
Nyerere amesema kuwa hakuna msanii hata mmoja ambaye anakidai Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na kusema mambo ambayo anasema Weme Sepetu kuwa
anakidai chama hicho ni uongo na uzushi mtupu.
Amesema
katika wasanii mbalimbali ambao huenda walilipwa pesa nyingi zaidi ni
Wema Sepetu pamoja na yeye na kusema wao pamoja na wasanii waliokuwa
wanaendesha kampeni ya 'Mama ongea na mwanao' ni wasanii ambao walilipwa
vizuri sana na Chama Cha Mapinduzi kuliko wasanii wengine wowote wale.
Steve
Nyerere anasema katika mkataba walioingia na Chama Cha Mapinduzi hakuna
sehemu mkataba huo unasema ukikamatwa na madawa ya kulevya, bangi
chama hicho kitakuja kukusaidia.
Pia
Steve Nyerere anakiri wazi kuwa sauti ambayo inazunguka kwenye mitandao
ya kijamii ni kweli ni sauti yake na alikuwa akiongea vile ili
kumridhisha mama yake na Wema Sepetu kwani wakati huo jambo hilo
lilikuwa ngumu kwake.
Post a Comment
karibu kwa maoni