Watu wanne wamefariki na saba kujeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi walipokuwa wanachimba dhahabu katika mgodi usio rasmi kijiji cha Itumbi Kata ya Matundasi Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema
Madusa amesema waliofariki ni pamoja na Simon Majaliwa(25)mkazi wa
kijiji cha Itumbi, Mazoea Mahona(25)mkazi wa Tabora,Benny
Bahati(23)mkazi wa Mapogolo Chunya na James Alinanuswe(26)mkazi wa
Tukuyu Rungwe.
Madusa amesema kuwa waliojeruhiwa ni Andrew Paul(26)mkazi wa Itumbi
,Marco Frederick(22)mkazi wa Itumbi,Isack James(30)mkaziwa Itumbi na
Hamisi Mwalyosi (25)mkazi wa Mapogolo.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Chunya amesema kuwa watu watatu walimbia baada
ya tukio hilo ili kukwepa mkono wa sheria. Miili yote imetambuliwa na
ndugu ambapo wamekabidhiwa kwa ajili ya taratibu za mazishi na majeruhi
wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Chunya wakipatiwa matibabu.Hata
hivyo Madusa amesema kuwa watu hao walivamia mgodi huo asubuhi februari
20 mwaka huu ambapo mmiliki wake hajafahamika na kuanza kuchimba dhahabu
bila kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha mvua.
Baada ya udongo kuporomoka juhudi za uokoaji zilianza na watu saba
walinusurika ambapo watatu walikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Chunya na
watatu walitokomea kusikojulikana. Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa
wananchi kuacha kuendesha shughuli za uchimbaji bila kibali na kuchukua
tahadhari hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha
mkoaani Mbeya.
Post a Comment
karibu kwa maoni