Kweli
nimeamini mapenzi hayana mwenyewe na huku waswahili husema ukistaajabu
ya Mussa…… hapo waweza malizia mwenyewe. Hii tunaiona kwa Mzee Willy
Kinyua (98) baada kufunga ndoa na Joyce Nyambura (88) baada ya wenza hao
kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 60.
Hehehe,
Wengine wetu wasipoona ndoa mapema hulalamika na kukata tamaa, Je
ungekuwa Joyce ingekuwaje baada ya kuishi na bwana huyo miaka hiyo 60,
hatuwezi kusema sana ila lahasha! yawezekana mzee Willy aliupanga huo
muda ndio wakati sahihi wa kumuona Mwanamke huyo.
Wanandoa
hao wamefunga ndoa katika Kanisa la Ubatizo lililopo Solai kwenye
Kaunti ya Nakuru nchini Kenya huku wakiwa na watoto 5, huku sasa
wakitembea kwa fimbo.
Aidha
Kinyua alisema kuwa alikuwa miongoni mwa waliopigana vita ya MauMau na
kwamba, ingawa alikuwa porini kwa miaka tisa, Nyambura hakumsaliti.
“Nampenda Nyambura, ni mwanamke mrembo ambaye kila mara amekuwa chanzo
cha nguvu zangu na kunitia moyo. Hajawahi kunisaliti.”
Kwa
upande wake Nyambura amesema, amefurahi kusheherekea ndoa yake kama
ambavyo kila mwanamke angependa iwe hivyo, huku akidai kuwa alimpenda
sana Kinyua na kwamba walikuwa wakiishi kwa imani.
Post a Comment
karibu kwa maoni