Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga amesema kuwa
Watanzania waliokuwa nchini Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka
taratibu na sheria za kuishi nchini humo.
Mahiga
amesema kuwa Watanzania hao wamefukuzwa Msumbiji baada ya kubainika
kuwa wanaishi nchini humo bila kuwa na pasipoti za kusafiria, vibali vya
kuishi na kutofuata vigezo walivyokuwa wamepewa na mamlaka husika ya
nchi hiyo.
Hayo
ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
ugeni unaotarajiwa kuwepo nchini Tanzania wa Rais wa Uganda, Yoweri
Museveni anayetarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya Kitaifa nchini
Februari 25 na 26, 2017.
Rais
wa Visiwa va Shelisheli, Mhe. Dannu Faure naye atawasili Tanzania kwa
ziara ya siku mbili kuanzia Tarehe 27-28, februari mwaka huu.
Post a Comment
karibu kwa maoni