Waandishi wawili wa Zimbabwe wamekamatwa kuhusiana na ripoti ya gazeti moja ilioelezea kwamba afya ya rais wa taifa hilo Robert Mugabe 'imedhoofika' alipoelekea nchini Singapore kwa kile afisi ya rais huyo ilisema ni zaira ya kimatibabu.
Muhariri wa gazeti la kibinafsi la NewsDay ,Wisdom Mudzungairi na mwandishi aliyeandika ripoti hiyo Richard Chidza hatahivyo wameachiliwa na ni sharti wajiwasilishe mahakamani.
Wakili wao Obey Shava amesema kuwa wameshtakiwa kwa kuhujumu na kutusi afisi ya rais.
Taarifa hiyo iliosema 'Mugabe yuko katika hali mbaya' ilinukuu duru zikisema kuwa rais huyo alisafirishwa kwa ndege siku ya Jumatano alfajiri.
Mugabe alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya mwaka 93 na amekuwa katika mamlaka tangu 1980.
Kulingana na chombo cha habari cha AP, watu wanaopatikana na hatia ya kumtusi Mugabe, uhudumia kifungo ijapokuwa kesi nyengine zimetupiliwa mbali.
Post a Comment
karibu kwa maoni