Liverpool imeiadhibu Arsenal ya Arsene Wenger kwa kichapo cha 3-1 .
Wakati Arsenal, wanachapwa mabao hayo Manchester United kuiptia kwa nyota Zlatan Ibrahimovic imetoka sare ya bao 1-1 na Bournemouth bao lililofungwa na Tyrone Mings uwanja wa Elbow.
Mechi hiyo ilikumbwa na visa vya ukosefu wa nidhamu uliomuhusisha mshambuliaji wa United Zlatan Ibrahimovic na Tyrone Mings wa Bournemouth.
Visa vyote viwili vilitokea mwisho wa kipindi cha kwanza cha mechi baada ya wachezaji hao kuonywa na refa Kevin Friend.
Alipewa kadi ya njano ambapo Friend aligundua ni yake ya pili na hivyobasi kutakiwa kutoka uwanjani.
Marcos Rojo aliiweka kifua mbele Manchester United kabla ya Bournemouth kusawazisha.
Baadaye mshambuliaji wa United Ibrahimovic alishindwa kufunga mkwaju wa penalti baada ya beki wa Bournemouth kuunawa mpira langoni.
Post a Comment
karibu kwa maoni