Baada ya kumtimua John McKinstry mwezi wa nane mwaka jana, timu ya taifa ya Rwanda almaarufu kama Amavubi wamemtangaza Mjerumani Antoine Hey kama kocha mpya wa kikosi hicho.
Akiongea na waandishi wa habari raisi wa chama cha soka cha Rwanda Vincent Nzamwita amesema wamempa timu Antoine Hey kwa ajili ya kuwapeleka katika mashindano yafuatayo ya AFCON pamoja na CHAN.
“Amepewa kazi maalum kwa ajili ya kufuzu michuano ya CHAN hapo mwakani, lakini vilevile tunaamini Antoine anaweza kukipeleka kikosi chetu katika michuano ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON alisema Nzamwita.
Kwa upande wake Antoine alisema anafurahia sana kuaminiwa na chama cha soka cha Rwanda na kuwaahidi kutokuwaangusha. “Nashukuru na najisikia faraja kupewa nafasi hii,tuna mechi ngumu lakini tutapambana kufudhu CHAN na AFCON”.
Antoine atapambana na Ivory Coast katika mechi za kufudhu AFCON kabla ya kuja Dar Es Laam kukabiliana na Taifa Stars mwezi July ambapo mshindi wa pambano hilo atakutana na timu ya taifa ya Uganda The Cranes.
Hey ameshawahi kuichezea klabu ya Schalke 04 lakini pia Birmigham City.Katika nyanja ya ukocha Antoine ameshazifundisha Lesotho,Gambia,Liberia na hatimaye sasa yuko Amavubi.
Wakati Amavubi wakimtangaza kocha mpya,habari toka Kinshasa ni tofauti kwa zinaeleza Thiery Forger amefungashiwa virago, Forger alikuwa kocha wa Tp Mazembe na ametimulowa baada ya Mazembe kuondolewa katika klabu bingwa Afrika.
Post a Comment
karibu kwa maoni