0
CaitlynHaki miliki ya pichaCHARLESTON ANIMAL SOCIETY
Mwanamume mmoja raia wa Marekani ambaye alifunga mbwa wake kwenye mdomo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.
William Dodson, mwenye umri wa miaka 43, anasema alimfunga mbwa huyo mdomoni kwa sababu alibweka sana. Ililazimu mbwa huyo kufanyiwa upasuaji mara kadha baada ya kupoteza sehemu ya ulimi wake.
Siku moja baada ya hukumu hiyo kutolewa, William Dodson pia alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, kwa mashtaka tofauti ya bunduki.
CaitlynHaki miliki ya pichaCHARLESTON ANIMAL SOCIETY
Vifungo hiyo viwili vitafuatana.
Kulingana na polisi William Dodson alimnunua mbwa hiyo kwa jina Caitlyn kwa dola 20.
CaitlynHaki miliki ya pichaFACEBOOK/CHARLESTON ANIMAL SOCIETY
Image captionCaitlyn
Dodson, ambaye alikuwa huru kwa dhamana wakati huo, alimfunga mbwa huyo nje baada ya kumfunga mdomo wake mara tisa.
Lakini mbwa huo alifanikiwa kutoroka mwezi Mei mwaka 2015, na alikuwa mgonjwa sana wakati alipatikana akirandaranda barabarani.
Kamba aliyotumia kumfunga mbwa hiyo ilizuia damu kufika hadi kwenye ulimi wake, na iliwachukua madaktari wa mifugo karibu saa 36 kuiondoa.
CaitlynHaki miliki ya pichaFACEBOOK/CHARLESTON ANIMAL SOCIETY
Image captionCaitlyn
Wakati huo chama cha wanyama cha Charleston, kibadilisha picha ya akaunti yake na kuweka picha ya mbwa hiyo, kama njia ya kuonyesha uzalendo.
Wamekuwa wakichapisha taarifa jinsi mbwa huyo anavyoendelea katika kisa hicho kilichoangaziwa kimataifa.
Caitlyn, alikuwa na umri wa miezi 15 wakati alipatikana na sasa amehitimu miaka mitano akiwa anaishi na familia tofauti.
CaitlynHaki miliki ya pichaFACEBOOK/CHARLESTON ANIMAL SOCIETY
Image captionCaitlyn

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top