Mke wa aliyekuwa mchezaji wa Ghana Michael Essien ameinunua klabu ya ligi ya tatu Como ,kulingana na klabu hiyo.
Akosua Puni Essien ameripotiwa kulipa pauni 206,000 katika mnada wa klabu hiyo iliofilisika.
Mmiliki mpya na timu yake sasa ana mpangowa kuimarisha kikosi cha kwanza pamoja na ile timu ya vijana kukuwa.
Wataweka juhudi za kuifanya kurudi katika Serie B na kukuza vipaji vya vijana waliomo.
Puni Essien amejielezea kuwa mfanyibiashara ,mshauri, mtu anayependa kusaidia na mama wa watoto watatu.
Como imeshiriki mara kadhaa katika ligi ya daraja la kwanza ya Seria A ,ikiwa imecheza sana kati ya 1984 hadi 1989 na hivi majuzi ikiwa 2002-2003 ambapo walishushwa daraja baada ya msimu mmoja.
Walishushwa daraja hadi ligi ya daraja la tano baada kufilisika.
Post a Comment
karibu kwa maoni