0
Mbunge wa Babati mjini Paulina Gekul akiwa nyumbani kwake Ngarenaro.[Picha na John Walter]
Mbunge wa babati mjini Mheshimiwa Paulina Gekul  amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumlinda kwani hakutegemea kuwa hai kwa jinsi ajali ilivyokuwa.
Akizungumza na Johnwalterhabari nyumbani kwake Ngarenaro jimbo la Babati mjini mkoani Manyara amesema kuwa kila jambo ni Mungu anapanga na kwa jinsi ajali ile ilivyotokea sikudhani kama tungekuwa hai mimi na dereva wangu'alisema Gekul mbunge wa jimbo la Babati mjini kwa tiketi ya Chadema.
Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumamosi akiwa katika ziara ya naibu waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina wakati akielekea kumalizia ziara yake kwa kutembelea ziwa Babati mjini Babati kwa upande wa Nangara ambapo pia chanzo cha maji kipo katika eneo hilo baada ya kumaliza kuzunguka katika kiwanda cha Perfume Siera na Dampo kuu la taka Sigino Pamoja na kutembelea gari la taka lilinunuliwa kwa kodi za wananchi wa mji wa Babati milioni mia mbili thelathini [230].
Mheshimiwa Mbunge jimbo la Babati mjini Pulina Philip Gekul  akiwa nyumbani kwake mjini Babati.Picha na John Walter
"Tulikuwa tunamalizia ziara katika jimbo langu lakini tulipotoka Hango Sinai baada ya kupata chakula tukawa tunaelekea ziwani na mimi nilikuwa wa mwisho katika ule msafara na tuliachana na msafara karibu na Zebra Cross hapo kati kati karibu na Machinga walipo,kwa hiyo tukawa tumeachwa mita chache,nilivyofika  Hangoni wakati tunaelekea Nangara mbele yetu alikatisha dereva Boda boda akiwa amempakia mtoto mdogo wakati huo mwendo wetu sio mkubwa sana na upande mwingine gari dogo linakuja ikabidi dereva apige honi ili boda apishe,boda boda alipisha lakini wakati dereva wangu anajaribu kupita, gari likavuta upande wa kulia na kuanza kuyumba likapaa hewani na kupinduka....wakati wote  huo nilifunga macho sikuataka kuoana kinachotokea nikisubiri tu kufa mimi na dereva wangu".
"Sio kila ajali ni Mungu ndio anapanga kwani sio watu waote wananipenda inawezekana kuna mkono wa mtu lakini mimi sintokata tamaa nitaendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo la Babati kwa kuwa wamenichagua,nawapenda sana wananchi wa jimbo la Babati na ninawathamini."aliongeza Pulina Gekul
Gari hilo lilipinduka upande wa dreva kisha likarudi upande mwingine alipokuwa ameketi Mbunge.
Hata hivyo dereva alijitahidi sana kwani hakumgonga yeyote wala hakugonga kitu chochote,alieleza Mbunge huyo.
Mbunge Paulina Gekul akizungumza na John Walter nyumbani kwake.picha na John Walter
 Kwa kweli namshukuru sana dereva wa Halmashauri japo simkumbuki lakini amenisaidia sana,alinipeleka hospitali na kuhakikisha vitu vyetu vinakuwa salama.
Hata hivyo Mbunge huyo wa jimbo la Babati mjini aliumia kichwani baada ya gari kukita chini na shingo yake kubanwa na mkanda.
Hata hivyo umuhimu wa kufunga  mkanda kwenye gari umeonekana kwani kama sio mkanda ule basi Mheshiwa Mbunge angetupwa nje na hata kukandamizwa na gari hilo na kuleta habari zingine za kilema au mauti.
Hapa ni sebuleni nyumbani kwa Mheshimiwa Paulina Gekul.Picha na John walter
Ametoa shukrani kwa mbunge wa Babati vijijini Jituson Chapus kwa kuwa karibu naye mpaka anatoka hospitaki pamoja na naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina kwa kuonyesha ushirikiano wao.
Aidha amewashukuru wakazi wa Babati,watanzania,wanachadema na wote waliokuwa wakifuatilia kwa muda wote kutaka kujua hali yake.
Imeandikwa na John Walter

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top