LG G6 ina rangi aina tatu |
LG imezindua simu mya ambayo skrini yake ni kubwa na ambayo inaweza kutumiwa njia tofauti kwa wakati mmoja.
Simu hiyo LG G6 ina mfumo wa 18:9 badala ya mfumo wa 16:9 ambao unatumiwa na simu nyingi.
Hii ina maana kuwa skrini hiyo inaonekana kubwa kuliko kawaida.
LG imekiri kuwa simu iliyozinduwa awali ya G5 ilishindwa kufikia malengo yake ya mauzo.
LG inasema kwa simu hiyo haiwezi kuathiriwa na maji wala vumbi
Simu hiyo ilizinduliwa mjini Barcelona kabla ya kuanza kwa mkutano wa simu za mkononi duniani.
Skrini ya LG G6 ina upana wa sentimita 14.5 ikilinganishwa na skrini ya sentimita 13.5 ya LG5.
Simu hiyo mya pia inawewa kuzamishwa ndani ya maji hadi muda wa nusu saa bila ya kukumbwa na tatizo lolote.
|
Post a Comment
karibu kwa maoni