Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Hidaya Maeda amesema takwimu za miezi miwili ya mwaka huu zinaonyesha kwamba wanafunzi 18 wa sekondari wamepata mimba.
Idadi hiyo ni kubwa na inaonyesha tatizo la wanafunzi kupata ujauzito wilayani humo limeendelea kuongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mwaka jana wanafunzi 62 walipata mimba, kati yao sita wakiwa ni wa shule za msingi na 56 walikuwa wakisoma sekondari.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Mjini Christina Mndeme amesema vita ya mimba za mashuleni ni ngumu na inahitaji kupingwa na watu wote ikiwamo wazazi, walimu, wanafunzi na jamii yote bila kujali kama ni wazazi au siyo wazazi.
Mndeme amesema hayo wakati akizindua kampeni ya “Niache Nisome, Magauni Manne” inayolenga kumsaidia mtoto wa kike kumaliza masomo na kufikia ndoto yake.
Kampeni hiyo inatambulisha Magauni Manne kuwa ni sare ya shule, joho la mahafali ya chuo, gauni la harusi wakati gauni la nne ni lile analiovaa mwanamke wakiwa mjamzito, ambavyo alisema wasichana wakienda kwa mtiririko huo watakuwa wamefikia ndoto zao.
“Wakati mwingine mapambano yetu yanakwamishwa na baadhi ya wazazi ambao huwafundisha watoto wao wasikubali kuwataja waliowapa ujauzito, wanawakana lakini kumbe wazazi wanakuwa wamemalizana wao kwa wao jambo ambalo halikubariki hata kidogo,” amesema Mndeme.

Post a Comment
karibu kwa maoni