Wakati Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ulipokuwa ukiendelea mkoani Dodoma, baadhi ya waliokuwa wachama na viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ACT-Wazalendo wamepokelewa rasmi na CCM baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho.
Viongozi hao waliojiunga na CCM leo wamesema sababu kubwa iliyopelekea na kufikia uamuzi huo ni utendaji kazi wa Rais na Mwenyekiti wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli.
Miongoni mwa wengi waliopokelewa leo ni pamoja na, Moses Machali Mbunge wa zamani wa Kasulu Mjini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi na baadae kuahimia ACT Wazalendo. Alitangaza kujiunga CCM Novemba mwaka jana ambapo leo amepokelewa rasmi. Dkt Yared Fubusa, Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Mkoa wa Kigoma na Mgombea Ubunge jimbo Kigoma Kaskazini (CHADEMA).
Mwingine ni aliyetangaza kujiunga na CCM na kupokelewa na Mkutano Mkuu leo ni, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Said Arfi.
Post a Comment
karibu kwa maoni