0
Watu wengi wamekuwa hawafahamu wafanyaje ili kutunza betri la simu ambayo ni jipya ili lisiwahi kuaribika. Kama wewe ni miongoni mwa watu hao nakusihi uweze kuambatana nami kwani nitakueleza namna ya kuchaji betri likiwa jipya ili lisiharibike mapema.

Mara tu baada ya kununu simu. Iwashe simu hiyo kisha angalia ina asilimia ngapi ya chaji. Baada ya kuona ina asilimia ngapi, unashauriwa kufanya yafutayo;

Kama ina  asilimia hamsini (50%) au zaidi  usiweke simu kwenye chaji bali unatakiwa kuitumia, mpaka chaji hiyo itakofika asilimia kumi (10%) ndipo uiweke kwenye chaji.

Mara baada ya kuweka kwenye chaji hakikisha unaichaji simu hiyo kwa muda wa masaa matatu ndipo uanze kuitumia tena. Kwani baada ya masaa matatu itakuwa imejaa vizuri kwa ajili ya matumizi.

Lakini endapo umenunua simu mpya au betri jipya mara tu baada ya kuwasha ukakuta ina chaji ambayo ina asilimia arobaini na tisa (49%) kushukua chini (49%-0%) tafadhari sana usiitumie simu au betri hilo, bali iweke chaji kwa muda wa masaa matatu ndipo uanze kuitumia simu hiyo.

Lakini jambo la muhimu na lakuzingatia ni kwamba kumbuka kuichaji simu yako kila wakati kila inafika chaji kwa kiwango cha asilimia kumi (10%)

Kufanya hivi kutakusaidia sana kuweza kulitunza betri lisiwahi kuaribika mapema.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top