0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesisitiza uhuru wa vyombo vya habari nchini huku akisema vyombo vya habari binafsi sio maadui ila ni miongoni mwa wadau wakubwa wa kujenga nchi.

Dkt. Shein ametoa kauli hiyo mjini Zanzibar wakati akizungumza na watendaji wote wakuu wa serikali ya Zanzibar wakiwemo mawaziri wake wote, wakuu wa mikoa na wilaya na wandishi wa habari wakati akifungua mjadala maalum wa uhuisano wa vyombo vya habari  na serikali uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi ambapo amesema vyombo vya habari binafsi sio mbadala wa vyombo vya serikali na sio kazi yao kuikemea serikali ila lengo ni kushirikiana na vyombo vya serikali katika kujenga nchi ambayo nao ni sehemu yao nawajibu wao.

Dkt. Shein ambaye amekuwa na uhuisiano mzuri na vyombo vya habari tokea ingie madarakani amewataka watendaji wake hasa mawaziri wasiwaogope waandishi wa habari na wasiwakwepe huku akiwataka waondoshe hofu na wawe msatari wa mbele kutoa taarifa ili wananchi wajue serikali waliyoichagua na kuipa nguvu ya kuongoza wanawatumikia vipi,kitendo cha kuwakimbia ni kusababisha ukweli kupotea na uwongo kutawala.

Mapema katibu mkuu kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Abdulhamid Yahya mzee amesema lengo la mjadala huo ni kujenga uhusiano wa serikali na wandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta ufanisi na uhusiano mzuri na serikali.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Zanzibar kukutana na wandishi wa habari wa serikali mbele ya mawaziri na watendaji wote wa serikali huku wandishi hao kupewa fursa ya kusema matatizo yao na kuliza kile ambacho kimekuwa kero katika utendaji wao wa kila siku.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top