0
Pilipili hoho siyo kitu kigeni masikioni na machoni mwetu, tunaijua na huwa tunaitumia majumbani mwetu,wengi wetu tunaitumia kama kiungo cha mboga na wengine hutumia katika kutengeneza kachumbari/salads ili kuleta radha na pengine kuipamba kachumbari ionekane ya kupendeza na kuvutia.

 Zifuatazo ndizo faida za pilipili hoho katika mwili wa binadamu;

1. Huzuia na kuondoa gesi tumboni,kwa wale matumbo yao hujaa jaa gesi hii inawafaa.
2. Hutibu kuwashwa koo na vidonda kooni.
3. Huimarisha kinga ya mwili,kutokana na kuwa na wingi wa vitamin c vitamin hii hupigana dhidi ya magonjwa na kujenga kinga imara ya mwili.
4. Hutibu kuvuja/kutoka damu puani wenye tatizo hili wanashauriwa kutumia hoho.
5. Ni kinga ya dhidi ya kansa,hasa kansa ya kibofu cha mkojo.
5. Husaidia kwa wenye matatizo katika mfumo wa upumuaji mfano asthma.
6. Hutibu magonjwa yote ya ngozi kama vile mba, chunusi na vipele.
7. Hutibu ugonjwa wa homa ya manjano.
8. Hutibu kuhara/kufunga choo.
9. Husaidia kucontrol presha ya kupanda(hypertension/high blood pressure).

Unachotakiwa kufanya ni;
Tengeneza pilipili hoho kisha chukua karoti. Katakata vipande kisha saga mchanayiko huo katika brenda. Kisha itatokea juisi ambayo itakudaidia katika kutibu magonjwa niliyoyaainisha hapo juu.

Unatakiwa kunywa juisi hiyo vikombe viwili mpka vitatu vya juisi hiyo kwa siku.
Lakini pia kama hatakuwa na uwezo wa kutengeneza juisi, unaweza ukatengeneza kachumbari kisha ukachanganya na pilipili hoho.

Muhimu zingatia;
Tumia hoho ambayo halijapikwa kwani ndio linashauliwa kuliwa hzaidi kwani linakua na virutubisho vingi zaidi.

Asante na endelea kutumia muungwana blog kwa elimu na habari mbalimbali.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top