0
Image may contain: one or more peopleMbunge wa Monduli [CHADEMA] ameandika ujumbe mzito katika ukurasa wake wa Facebook akiwagusa viongozi wanaowatumia askari polisi vibaya.
Katika ujumbe huo Kalanga japo hakutaja mtu ila anamlenga mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliyeagiza Polisi kuwakamata viongozi mbali mbali akiwemo Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro walipokwenda kutoa rambi rambi za pole kwa familia zilizokumbwa na msiba ulitokana na ajali ya gari la Luck Vicent ya Arusha.
"Matumizi mabaya ya jeshi la polisi dhidi raia wa nchi kwa kuwakamata watu hovyo na kuwaandikia kesi za hovyo inajenga taswira hasi wa raia dhidi ya serikali yenyewe dhidi ya ccm yenye dhamana na dhidi ya Rais mwenyewe.
Kwamba kama ninyi hamtakemea mambo haya maanake wana baraka zenu.
Hatuna ugomvi na polisi lakini tuna ugomvi ja wale wanaowatuma polisi"aliandika Julius Kalnga mbunge wa jimbo la Monduli.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top