Serikali leo imerejea kauli yake ya kuhakikisha watu wanaofanya mauaji ya polisi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika wilaya za Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa operesheni maalum inayoendelea katika wilaya hizo ni lazima itoe matokeo yatakayomhakikishia kila mwananchi maisha salama ndani ya nchi hii.
Ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua kambi maalum ya operesheni ya kuwatafuta wauaji wa baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wilayani Kibiti, akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Pwani ambaye pia ni mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo.
Katika maelezo yake, Waziri huyo wa mambo ya ndani amesema hisia zilizokuwepo kwamba pengine mauaji hayo yanahusishwa na katazo la biashara ya mazao ya misitu ukiwemo mkaa, misimamo ya kidini, Ujambazi ama ugaidi siyo za kweli, bali ni mchezo uliobuniwa na kundi la watu kwa sababu ambazo haziko wazi na kwa hiyo ni lazima vitendo hivyo vikomeshwe mara moja.
Post a Comment
karibu kwa maoni