0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar kupitia Mjini Dar es salaamu kuelekea Amman Nchini Jordan kuhudhuria Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Forum – WCF} la Siku Tatu litakalohudhuriwa na zaidi ya Wajumbe 2,000 kutoka Nchi 58 Duniani.
Balozi Seif  anamuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo la Kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika litakaloshirikisha Vingozi Wakuu wa Nchi, Wafanyabiashara,wamiliki wa Makampunni ya Kimataifa, Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia, Mashirikia ya Kimataifa, Wana Habari pamoja na Vijana.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ZanzibarBalozi Seif  Ali Iddi aliyefuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi ameagwa na Mwaziri, baadhi ya Watendaji Wakuu  wa Serikali pamoja na
Viongozi wa Kisiasa.
Balozi Seif akiagana na Viongozi mbali wa Serikali na Taasisi za Umma kuelekea Nchini Jordan kwenye kumuakilisha Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufili kwenye Tamasha hilo la siku Tatu linaloanza Tarehe 19 Mei 2017.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Mjumbe wa Baraza la Mainduzi ambae pia ni Waziri asiye na Wizara Maalum Mh. Said Soud Said kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume akiondoka kupitia Dar es salaam kwa safari ya kuhudhuria Tamasha la Uchumi la Dunia { World Economy } linalotarajiwa kufanyika Amman Nchini Jordan.
Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif ameongozana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar  Balozi Amina Salum Ali, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.
Tarehe 19 Mei Balozi Seif na Ujumbe wake atashiriki Washa ya Utalii itakayojikita zaidi katika masuala ya Kujenga Uchumi kwa Mataifa ya Mashariki ya Kati na yale ya Kanda ya Afrika  ili kuona njia gani zinaweza kutoa fursa za ajira kwa Vijana kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa Warsha  itakayofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Kempisk
Mjini Amman Jordan.
Jukwaa hilo la Uchumi Duniani litafunguliwa na Kiongozi wa Jordan Mfalme wa Pili Abdullah  Bin Al-Hussein asubuhi ya Tarehe 20 Mei kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa King Hussein Bin Talal katika Bahari Nyeusi.
Baadawe Waziri wake anayehusika na Mipango na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa pia Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdullah Bwana Imad Fakhoury atapata wasaa wa kuwasilisha  mpango wa maendeleo wa
Taifa hilo.
Mpango huo umekuja kufuatia  mabadiliko makubwa ya uchumi yaliyofanywa na Nchi hiyo ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita  pamoja na kutafuta mbinu ya kupata utulivu na Amani wa Mashariki ya Kati na Kanda ya Afrika  kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi lililosababishwa na vita kwenye maeneo hayo.
Jordan imekuwa  muandaaji maarufu wa Jukwaa la Dunia la Uchumi { World Economy Forum }kwa takriban mara Tisa sasa na 16 kwa Kanda na Mashariki ya Kati ya Kaskazini mwa Afrika ambapo Viongozi wa Mataifa ya palestina, Misri, Kosovo, Iraq, Tanzania  na Morocco wanatazamiwa kushiriki Jukwaa hilo.
Mabadiliko makubwa ya uchumi yaliyofanywa na Jordan ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita yameliwezesha Taifa hilo la kiarabu kufungua milango ya Uwekezaji katika sekta za Nishati, Usafiri, Mipango ya Maendeleo ya Miji, huduma za Maji safi, Miundombinu ya Mawasiliano, Utalii pamoja na Mtandao wa Mawasiliano wa Kompyuta { ICT }.
Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum – WCF} limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake  Profesa Klaus Schwab huko Davos, Switzerland.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa 9ili wa Rais wa Zanzibar
17/5/2017.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top