0
Takribani siku mbili sasa kumekua na taarifa zisizo rasmi ndani ya mitandao ya kijamii kuhusiana na kile kilichodaiwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Comrade Abdulrahman Kinana kujiuzulu wadhifa huo ndani ya chama.
Aidha taarifa hizo zilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa Chama cha Mapinduzi kipo katika wakati mgumu kuweka wazi kuhusiana na kujiuzulu kwa Katibu Mkuu huyo.
Habari za uhakika zilizotolewa na Katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho Nd. Humphrey Polepole ni kuwa Kinana hajajiuzulu nafasi hiyo na kwasasa yeye (polepole) pamoja na Kinana wapo nchini Angola wakipeleka ujumbe wa CCM  mpya kwa vyama rafiki.
Polepole aliyasema hayo kupitia kwenye mtandao wa Twitter akimjibu mmoja wa waliomuuliza kuhusiana na ukweli wa jambo hili “Kazi yao kuzusha uongo kila siku, mimi, Ndg. Lubinga na Ndg. Kinana tuko Angola kikazi, huko tumepeleka ujumbe wa CCM mpya kwa vyama rafiki” Aliandika Polepole

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top