0

Taasisi na mashirika mbalimbali yametakiwa kujitokeza kusaidia wazee wanaoishi katika kituo cha kulelea wazee kilichopo Babati Manyara kinachokabiliwa na changamoto mbalimbali.

 

Wito huo umetolewa na mlezi wa kituo cha kuwalea wazee kilichopo kijiji cha Sarame kata ya Magugu Babati mkoani Manyara Samson Munuo wakati akizungumza na redio Manyara fm na kueleza kuwa zipo changamoto nyingi zinazokikabili kituo hicho ikiwemo gari kwa ajili ya kusaidia shughuli za kituoni hapo.

Kituo hicho cha kuwalea wazee kilianzishwa mwaka 1975 wakati huo mkoa wa Manyara ikiwa ni seheem ya mkoa wa Arusha,sababu ya kuwekwa kituo katika eneo la Magugu ni kutokana na hali ya hewa ya joto katika eneo hilo inayoendana na afya za wazee.

Na hata baada ya Manyara na Arusha kujitegemea bado huduma zimeendelea kutolewa katika kituo hicho kilichopo Manyara na kinahudumia mikoa yote miwili.

Mpaka sasa kituo kinawalea wazee 13,kati ya hao 10 wakiwa ni wanaume na 3 ni wanawake.

Kituo kina uwezo wa kuchukua wazee 36 na wakati kinaanzishwa kilikuwa na hekari 65 lakini kutokana na changamoto za hapa na pale zimebaki hekari 17 baada ya serikali ya kijiji kugawa.

Kituo kipo kilomita tatu na nusu kutoka kituo cha mabasi Magugu.

 

 

 

CHANGAMOTO

Huduma za afya,

Usafiri

Mavazi na chakula

Uchache wa watumishi

Nishati ya mwanga[umeme]


Mwanafunzi wa shule ya msingi Matwiga Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya aliyetambulika kwa jina la Daudi Kaila amefariki dunia baada ya kufungiwa katika chumba cha stoo ya shule na mwalimu Mkuu wao.


Inasemekana Mwalimu Mkuu huyo aliwafungia wanafunzi wawili kwa zaidi ya masaa mawili kwenye chumba hicho cha stoo akiwepo Daudi Kaila na mwenzake Felix Samweli ambaye yeye amenusurika kifo. Sababu kubwa mwalimu kuwafungia wanafunzi hao ilikuwa kuwaadhibu kutokana na wanafunzi hao kutohudhuria shule kwa siku tano.

Kufuatia tukio hilo kutokea walimu wa shule hiyo wamekimbia kusikojulikana kuokoa maisha yao kutoka kwa wananchi wenye hasira kali

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top