Michuano ya kombe la mabara
itaendelea tena leo hii kwa michezo miwili ya kundi A kuchezwa, wenyeji
Urusi watashuka katika dimba la Otkrytiye Mjini Moscow, kucheza na
Ureno .Na mchezo wa pili wawakilishi wa bara la Afrika katika michuano hiyo timu ya Cameroon watashuka katika dimba la Fisht Olympic kupepetana na New Zealand , mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Bakary Gassama kutoka Gambia.
Urusi ndio vinara wa kundi A wakiwa na alama tatu baada ya kupata
ushindi dhidi ya New Zealand, Ureno na Cameroon wao wana alama moja moja
na New Zealand wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja.
Post a Comment
karibu kwa maoni