0
Rais John Pombe MagufuliRais wa Tanzania John Magufuli ameshutumiwa kwa matamshi yake kwamba wasichana wanaojifungua hawafai kuruhusiwa kurudi shule.
Ombi la mitandao ya kijamii limewekwa huku shirika moja la wanawake barani Afrika likitoa hamasa ya kumtaka rais Magufuli kuomba msamaha kwa matamshi hayo.
Bwana Magufuli aliwaonya wasichana wa shule katika mkutano wa hadhara siku ya Jumatatu kwamba ''unaposhika mimba mambo yako yamekwisha''.
Sheria iliopitishwa mwaka 2002 inaruhusu kutimuliwa kwa wasichana waliotungwa mimba wakiwa shuleni.
Sheria hiyo inasema kuwa wasichana wanaweza kufukuzwa shuleni kwa ''makosa yanayokiuka maadili na ndoa''.
Makundi ya haki ya wanawake yamekuwa yakiishinikiza serikali kubadilisha sheria hiyo.
Magufuli ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika mji wa Chalinze ,takriban kilomita 100 magharibi mwa mji wa Dar es Salaam alisema kuwa kina mama hao wachanga hawatasoma vyema iwapo wataruhusiwa kurudi shule.
Baada ya kupiga hesabu ,atamtaka mwalimu wake kwenda nje ili kunyonyesha mwanaye anayelia.
Alisema kuwa wanaume wanaouwatunga mimba wasichana wa shule pia nao wanapaswa kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 30 na kuweka nguvu zao walizozitumia kuwatunga mimba wasichana hao kulima wakiwa jela.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top