Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Babati [BAWASA] kupitia mtaalamu wake wa ufundi Onores Sebastian wamesema kuwa wapo tayari kuongeza vituo Vya maji katika kijiji cha Gadwet endapo wanakijiji hao watakuwa tayari kuvuta maji kwenye nyumba zao.
Hatua hiyo
inakuja mwezi mmoja baada ya wanakijiji hao kupitia redio manyara kuiomba
Halmashauri ya mji wa Babati na mamlaka hiyo kuwaongezea vituo vya maji.
Wakazi wa
kijiji cha Gadwet kata ya Sigino Babati mjini kwa sasa wanategemea kituo kimoja tu, kupata maji hivyo kutumia muda mwingi kufuata maji hayo.
Kituo hiki kilishuhudia
wakina mama na watoto wakitoka umbali zaidi ya kilomita 3 kufuata maji.
Wamesema
kuwa shughuli zao nyingi zinakwama kutokana na kutumia muda mwingi kwenda
kufuata maji.
Mwenyekiti
wa kitongoji cha Gadwet Samwel Gwandu licha
ya kuishukuru mamlaka ya maji safi na mazingira Babati BAWASA ameeleza kuwa changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni
msongamano katika kituo.
Post a Comment
karibu kwa maoni