0


Responsive imageWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wawekezaji kuwekeza katika maeneo ya vijijini ambako kuna wahitaji wengi zaidi wa huduma za afya.
Waziri Ummy amesema hayo Jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha watoa huduma wa vituo vya afya na binafsi nchini -APHTA ulioshirikisha watoa huduma za afya, wamiliki wa vituo vya afya na wataalamu kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Mkutano huo umefunguliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dokta  Jakaya Kikwete ambaye amesema changamoto zinazoikabili sekta ya afya ni nyingi hivyo sekta binafsi zinapaswa kuwasaidia wananchi wa kawaida kupata bima za afya. 
Amesema serikali imepanga kupunguza vifo vya mama na mtoto kutoka vifo 556 kati ya akina mama 100,000 hadi kufikia nusu yake ifikapo mwaka 2020.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani -WHO za mwaka 2016 Tanzania ni nchi ya 150 kati ya nchi 188 katika utoaji wa huduma za afya huku ikiongoza kwa wastani wa umri wa kuishi ikiwa na miaka 65 katika ukanda wa Afrika Mashariki

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top