Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia
anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird,
wakibadilishana hati (mkataba) ya mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani
milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari
kupitia mpango wa lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), jijini Dar es
Salaam.
|
BENKI
ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani
milioni 80 kwa ajili ya kusaidia mpango wa Serikali wa miaka 11 wa Elimu bila
malipo kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari nchini.
Kiasi
hicho cha fedha ni nyongeza ya Dola milioni 122 zilizotolewa na Benki hiyo
katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa maboresho ya elimu kupitia Mpango wa
Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa-BRN, uliolenga kuondoa changamoto za elimu
nchini.
Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na
Burundi, Bella Bird amesema wakati wa utiaji saini mkataba wa nyongeza ya fedha
hizo kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James,
kuwa nyongeza ya Dola milioni 80 imetokana na Benki hiyo kuridhishwa na namna
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dokt. John Pombe Magufuli,
ilivyosimamia kikamilifu mpango huo wa utoaji elimu bure na kuwanufaisha
wanafunzi wengi wakiwemo wanaotoka katika familia masikini.
Amesema
kuwa uamuzi huo umesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na elimu
ya msingi, kuongezeka kwa ufaulu, wanafunzi kujua maarifa ya hesabu, kusoma na
kuandika, utoaji wa ruzuku ya elimu kwa wakati, hatua ambayo pia
imesababisha kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa miundombinu ya shule,
changamoto ambazo anaamini zinapungua kupitia mkopo huo wenye masharti nafuu.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James ameishukuru Benki ya Dunia
kwa kutoa fedha hizo ambazo amesema zitasaidia kwa kiasi kikubwa mipango ya
Serikali ya kuboresha elimu nchini na kuondoa changamoto zinazoukabili mpango
huo likiwemo ongezeko hilo kubwa la wanafunzi.
Bw.
James ameeleza kuwa fedha hizo zitasaidia ujenzi wa miundombinu ya madarasa,
ubora wa eimu, ukaguzi wa shule, upelekaji wa walimu, na kuwasaidia wanafunzi
wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata haki hiyo ya msingi ya elimu.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Simon Msanjila, amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa
elimu wa lipa kulingana na matokeo upitia mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za
Marekani milioni 122 zimetumika kujenga madarasa 1,400, matundu 3,390 ya vyoo,
mabweni 261, majengo ya utawala 9, mabwalo ya chakula 9 nyumba za walimu 11,
uchimaji wa visima vya maji katika shule nne na kukarabati vyuo vya ualimu.
Amesema
kuwa mkopo mpya wa dola za Marekani milioni 80 uliotolewa na Benki ya
Dunia hata kabla ya awamu ya kwanza ya mradi huo kumalizika hapo mwakani,
umeonesha nia ya dhati ya Benki ya Dunia kusaidia maendeleo ya elimu nchini.
Post a Comment
karibu kwa maoni