Takriban watu watano wa kampuni ya kuchimba mafuta waliuawa, kwa mujibu wa chuo cha Maiduguri.
Wanajeshi pia waliuawa wakati wa uvamizi huo.
Idadi hiyo kubwa ya vifo ni pigo kwa serikali ambayo inasisitiza kuwa kundi la Boko Haram limeshindwa.
Takriban watu 20,000 wameuawa na maelfu ya wengine kutekwa tangu Boko Haram ianzishe harakati zake mwaka 2009.
Katika kisa kibaya zaidi Boko Haram waliteka wasichana 276 kutoka shule ya wasichana kaskazini mashariki mwa Nigeria ya Chibok mwaka 2014.
Tangu wakati huo wamewaachili zaidi ya wasichana 100 kubadilishana na wapiganaji.
Taarifa za kina kuhusu kile kilichotokea siku ya Jumanne hazijulikani, huku ripoti za awali kutoka kwa jeshi, zikisema kuwa watu ambao walitekwa waliokuwa ni wakifanya kazia katika chuo cha Maiduguri waliachiliwa,.
Siku ya Jumanne jeshi lilisema kuwa miili ya wanajeshi 9 na raia mmoja ilikuwa imepatikana.
Lakini sasa chuo kikuu kimesema kuwa takriban wafanyakazi watano wakiwemo wasomi wawili na dereva waliuawa wakati msafara wao uliokuwa chini ya ulinzi mkali, ulikuwa ukirejea mjini Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria
Wengine kadha hawajulikani waliko.
………………………………..
Bunge la waakilishi liliidhinisha mswaada huo
mapema wiki hii kwa kura nyingi.Baada ya mswaada huo kupita katika mabunge yote sasa utapelekwa kwa Rais Donald Trump kuwekwa sahihi.
Lakini bwana Trump anataka kuboresha uhusiano na Urusi na anaweza kuukataa licha na uungwaji mkono uliopata.
Vikwazo hivyo ni vya kuiadhibu Urusi zaidi kufuatia hatua za kulimega eneo la Crimea kutoka Ukrain mwaka 2014.
Lakini mjadala kuhusu vikwazo hivyo vipya unafanyika huku uchunguzi kuhusu hatua za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 ukiendelea.
Bwana Trump mara nyingi amekana kuwa Urusi iliingilia uchaguzi huo kusaidia kampeni yake.
Waandishi wa masuala ya siasa wanasema kuwa ikiwa Trump atajaribu kuukataa mswaada huo basi itakuwa ishara tosha kuwa anaiunga mkono sana Urusi.
……………………….
Mpango wa kuanzisha ukanda maalum ambao
utakua unahusika na utoaji misaada hauna maendeleo mazuri.Mkuu wa shirika la kutoa misaada amesema kuwa kwa mwezi huu hakuna msaada uliotolewa kwa sehemu 11 zilizoathirika na vita.
Ameituhumu serikali ya Syria kwa kuzuia misaada ya kibinaadam, huku pia akitaja makundi ya upinzani kwa serikali kama sababu ya kuwarudisha nyuma.
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dokta
Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika mitaa ya mji wa Dodoma na
kubaini baadhi ya wafanyabiashara hawatumii ipasavyo mashine za kieletroniki za
kukusanyia kodi ya Serikali-EFDs na kuwaonya wafanyabiashara kote nchini kuacha
mchezo huo.
Dkt. Mpango aliyeambatana na baadhi ya
maofisa wa Mamlaka ya Mapato hapa nchini-TRA mkoa wa Dodoma amebaini baadhi ya
wafanyabiashara hao wasio waaminifu hawatoi risiti huku wengine wakiandika
kiwango kidogo cha fedha kwenye risiti hizo.
Mmoja wa wafanyabiashara aliyekumbana
na mkono wa Waziri Dokta Mpango, ni Bwana ISDORI SHIRIMA ambaye amekiri kufanya
makosa ya kutotumia mashine hizi ipasavyo
“naomba unisamehe Mheshimiwa, sitarudia
tena unajua sisi vijana tunabangaiza, lakini nimebaini nimefanya makosa”
aliomba msamaha Bw. Shirima
Hata hivyo Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka
ya Mapato Tanzania-TRA mkoa wa Dodoma, kufanya ukaguzi wa kina wa mahesabu ya
mfanyabiashara huyo ili kubaini kiwango cha kodi alichokwepa na kumchukulia
hatua stahiki.
Aidha, Dokta Mpango ameiagiza Mamlaka
ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Dodoma kuwapeleka ofisini kwake mawakala wote
mkoani humo wanaosambaza mashine za kieletroniki za kukusanyia mapato EFDs
baada ya kubaini kuwa zaidi ya mashine 100 zimeharibika na hazitumiki tangu
jana.
“Kuna kitu sikielewi na hakiingii
akilini, inakuwaje mashine ziharibike kwa kiwango hicho, mashine 100 kuharibika
kwa siku mbili ni nyingi na ina maana nimekosa mapato mengi” alielezea kwa
masikitiko Dkt. Mpango.
Aliagiza mawakala wote wanaosambaza ama
kuuza mashine hizo wakutane naye ofisini kwake mjini humo ili kubaini tatizo na
kuongeza kuwa haiwezekani wafanyabishara walipie mashine hizo zaidi ya mwezi
uliopita lakini hawapelekewi hali inayozidi kuikosesha Serikali mapato yake.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara
wamepongeza uamuzi wa Serikali wa kulivalia njuga suala la kodi na kwamba wako
tayari kuiunga mkono Serikali kwa kutoa risiti wanapouza bidhaa na kudai risiti
zenye viwango sahihi vya manunuzi waliyoyafanya ili kuijengea Serikali uwezo wa
kuihudumia jamii.
Dokta Mpango ametembelea pia baadhi ya
vituo vya mafuta mjini humo na kuwakumbusha wamiliki wote wa vituo vya mafuta
kuzingatia agizo la Serikali linalowataka wafunge mashine maalumu za
kielektroniki zinazofungwa kwenye pampu za mafuta ndani ya siku 14 ambazo ziko
ukingoni.
Post a Comment
karibu kwa maoni