0
TAMBUA JINSI MNYAMA HUYO ANAVYOISHI NA CHAKULA ANACHOKULA.
Ukifika Babati mjini kando ya ziwa Babati utaona viboko hao wakati wanaota jua na kula majani pembezoni mwa mto.
Wakati wa usiku Viboko hawa huwa wanatembea maeneo ya nchi kavu kujitafutia chakula na inapofika alfajiri wanarejea katika maeneo yao ya majini.

Mnyama Kiboko ndani ya Ziwa Babati-Manyara Tanzania.
Kiboko huishi kwenye maji ya mito na maziwa lakini ana uwezo wa kutembea kwenye nchi kavu mbali na maji. Chakula chake ni majani.
Kimo cha mbegani kinafikia mita 1.5 na urefu wake hadi mita 4.5. Uzito wake ni kati ya kilogramu 2700 na 4500 kg. Hivyo kiboko inashindana na kifaru juu ya cheo cha kuwa mnyama mzito wa pili kwenye nchi kavu baada ya tembo. Akikimbia hufikia mwendo wa kilomita 48 kwa saa ingawa kwa muda mdogo tu.
Kiboko akiwa nchi kavu.
Viboko huishi majini na nchi kavu, hasa kwenye maziwa na mito ambako viboko dume huishi kwenye sehemu kubwa ya mto na jike na watoto 5 mpaka 30.
 Wakati wa mchana hubaki wametulia kwa kukaa ndani ya maji au matope; kuzaliana na kuzaa watoto vyote hutokea ndani ya maji.
Kundi la viboko mtoni Luangwa (Zambia)
Kundi la viboko likiwa katika mto Luangwa nchini Zambia.
 Hujitokeza nyakati za giza kula nyasi. Wakati viboko hupumzika pamoja ndani ya maji, wakati wa kula nyasi hutawanyika na hakuna mipaka.
Licha ya kufanana kimaumbile na nguruwe na wanyama wengine wenye kwato nne, wanyama ambao wanachimbuko moja la karibu la uhai ni "sesataseani", (nyangumi, porpoises nk.) ambako walitoka zaidi ya miaka milioni 55 iliyopita. Mnyama wa kale asili ya nyangumi na kiboko aligawanyika kutoka jamii nyingine za wanyama wenye kwato nne mnamo miaka milioni 60 iliyopita.
Mabaki ya kale zaidi ya kiboko ni ya jenasi Kenyapotamus katika Afrika, wa tangu miaka milioni 16 iliyopita.
Kiboko anatambulika kwa kinywa na meno yake makubwa, mwili usio na nywele, miguu mifupi na umbo kubwa.
 Ni mnyama wa ardhi wa tatu kwa ukubwa akiwa na uzito (kati ya tani 1.5 na 3.5), nyuma ya faru mweupe (tani 1.5 mpaka 4 ) na tembo (tani 3 mpaka 7 ).
Licha ya umbo lake la kujaa na miguu mifupi, kiboko huweza kumshinda mbio binadamu kwa urahisi. Kiboko pia katika mbio fupi wanafikia mpaka kasi ya km 29/saa.
Kiboko ni miongoni mwa viumbe ambao ni wakorofi kuliko wote an husemekana kama ni mnyama kali kuliko wote Afrika.
 Kuna kadiri ya viboko 125,000 mpaka 150,000 katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara; Zambia 40,000 na Tanzania 20,000 mpaka 30,000.[1] Viboko bado wapo kwenye tishio la kutoweka kutokana na kutoweka kwa uoto na ujangili kuwinda nyama yao na meno yao chonge ya vipusa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top